MBUNGE wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa jengo jipya la kupumzikia kwa ndugu,jamaa na marafiki wa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
MBUNGE wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde,akiwa na wananchi akishiriki kuchimba msingi mara baada ya kuzindua ujenzi wa jengo jipya la kupumzikia kwa ndugu,jamaa na marafiki wa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
MBUNGE wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde,akizungumza mara baada ya kuzindua ujenzi wa jengo jipya la kupumzikia kwa ndugu,jamaa na marafiki wa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
….
MBUNGE wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde ,amezindua ujenzi wa jengo jipya la kupumzikia kwa ndugu,jamaa na marafiki wa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza leo Septemba 19,2024 jijini Dodoma mara baada ya kushiriki uzinduzi huo Mavunde amesema ataendelea kuimarisha miundombinu ya Afya mkoani humu ili wananchi waweze haki kupata huduma bora za Afya.
Amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo utasaidia kulinda usalama wa ndugu zao wakati wakiwa wanawangojea wagonjwa pindi wakipatiwa matibabu yao.
“Ndugu zangu leo tumeanza ujenzi huo na picha zake mmeziona zitakavyokuwa jengo hilo tutalijenga kwa kulitenganisha sehemu ya akina baba na akina mama na litakuwa la kisasa na lenye ubora mkubwa kwa wananchi wa Dodoma na wananchi wengine kutoka sehemu mbalimbali watakaokuja kupata matibabu katika hospitali hiyo.”amesema Mhe.Mavunde
Pia ameeleza kuwa jengo litakapokamilika litakuwa na sehemu mbalimbali za burudani ambapo atawafungia TV kubwa ili waweze kupata huduma bora wakiwa katika eneo hilo,atajenga vyoo vya kisasa kikubwa
Amesema kuwa ataendelea kushirikiana na uongozi wa hospitali hiyo katika kuboresha miundombinu kama mlivyoniomba kwenye taarifa yenu mtakumbuka miaka mitatu niliwaleta madaktari bingwa latika hospitali hii kwa kutoa huduma bure kwa ajili ya upasuaji wa macho na huduma nyingine.
“Pale nje ya geti letu lipo eneo ambalo huwa wanakaa wananchi ambao asilimia kubwa hawaishi katika jiji la Dodoma wananchi hao wanatumia jengo hilo kupumzikia kwa ajili ya kwenda kuwaona wagonjwa wao punde muda mnapofika wapo baadhi yao hawana sehemu ya kulala ,hawana makazi Dodoma na hawawezi kurudi walipotoka kwa sababu ni mbali maisha yao yamekuwa pale kwenye jengo wakina baba,Mama na watoto wanachanganyikana ambapo ni kinyume na maadili yetu ya Kitanzania.
Aidha amempongeza Mhe.Rais Samia kwa kazi kubwa ya uwekezaji katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambapo imebadilika kwani mazingira ya sasa yapo tofauti na zamani vifaa vingi vimeletwa na huduma mbalimbali zinapatikana katika hospitali hiyo.
Hata hivyo amemuomba Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma kuongea na Mkurugenzi wa jiji kutowaondosha wa Mama lishe wanaoendesha shughuli zao pembezoni mwa hospitali hiyo bali waboreshewe mazingira ya kazi yao.
Baadhi ya ndugu wa wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, wamesema ujenzi wa jengo maalumu kwa ajili ya kupumzikia ndugu wa wagonjwa litakuwa sehemu salama kwao ikilinganishwa na hali iliyopo sasa.