Na Lucas Raphael,Tabora
Utoro wa baadhi ya wanafunzi wa kujificha vichakani,kuokota makopo, vyuma chakavu kwa ili ya kuuza na kufanyakazi za vibarua kwenye mgodi wa Dhahabu wa Matinje Uliopo wilayani Igunga Mkoani Tabora.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kiloleni Evangeline Materu wakati wa maghafali ya kwanza ya wanafunzi 28 waliomaliza elimu ya msingi mwaka huu .
Alisema kwamba hali iliyosababisha wanafunzi kusafiri umbali wa kilomita Nne kwenda katika shule ya Msingi Mama Matinje kumekoma baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa shule ya Msingi dada ya Kiloleni iliyopo karibu na Mgodi huo kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 360.
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Matinje Lukas Mchele aliipongeza serikali awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukamilika shule hiyo iliyoanza kutoa elimu rasmi January mwaka huu wa 2024 .
Alisema wamba hadi sasa inazaidi ya wanafunzi 600 wakiwamo wa darasa la awali, darasa la kwanza na wa darasa la pili hadi la saba ambao wahamishiwa hapo kutoka shuleya Msingi Matinje hivyo kunusuru janga la watoto kukosa elimu ambao ni haki yao ya Msingi.
Kupitia mahafali ya kwanza ya wahitimu 28 wa darasa la saba waliohamishiwa shule ya Msingi Kiloleni kutoka shule Mama ya Matinje, wawekezaji na wachimbaji mbalimbali wa mgodi huo, wakiongozwa na Mwekezaji Peter Mashili wamechangia zaidi ya shilingi milioni 4. 5 kwa ajili ya kuunganisha umeme,kununua Mashine ya kuchapishia na vifaa mbalimbali vya shule ikiwa ni hatua ya kuunga mkono juhudi hizo za serikali
Pia wazazi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na serikali tayari wameanza mikakati ya kujenga nyumba za walimu ili waweze kukaa karibu na shule hiyo ikiwa ni hatua ya kuwaondoloa atha ya kupanga nyumba zilizopo katika mgodi huo