Mstahiki Meya wa baraza la Manispaa wilaya ya kaskazini ‘A’ Machano Fadhil Machano (Babla), alipokua akifungua mafunzo ya mabadiliko ya sheria za kodi 2024-2025 kwa wafanya biashara na wananchi wa mkoa wa Kaskazini Unguja
NA FAUZIA MUSSA
Wananchi wa Mkoa wa kaskazini Unguja wametakiwa kuendelea kulipa kodi ili kusaidia kuimarisha maendeleo ya mkoa huo.
wito huo umetolewa na Mstahiki Meya wa baraza la Manispaa wilaya ya kaskazini ‘A’ Machano Fadhil Machano (Babla), alipokua akifungua mafunzo ya mabadiliko ya sheria za kodi 2024-2025 kwa wafanya biashara na wananchi wa mkoa huo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), katika ukumbi wa mikutano wa baraza hilo Mkokotoni.
Alisema mabadiliko ya kimaendeleo yanayoonekana Nchini yametokana na misingi ya ulipaji kodi, hivyo ni vyema wafanyabiashara na jamii kwa ujumla kulipa kodi Kwa hiari, Jambo ambalo alilitaja kuchochea upatikanaji wa huduma za jamii mkoani humo na taifa kwa ujumla.
aidha alisema kufanya hivyo pia ni sehemu ya kuunga mkono harakati za maendeleo zinazosimamiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Husein Ali Mwinyi.
Hatahivyo aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi wengine katika kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yao.
Mkuu wa Kitengo cha habari uhusiano na huduma kwa walipakodi ZRA, Makame Khamis Moh’d, alisema mabadiliko ya Sheria ya kodi yametokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupata sheria za kodi zinazo kwenda na wakati, hali ya uchumi wa nchi, mwenendo wa ukuaji wa baishara, mabadiliko ya teknolojia pamoja na changaomoto katika utekelezaji wa sheria.
Alibainisha kuwa mabadiliko hayo yalizingatia maeneo ya watu wenye mahitaji maalumu,uwekezaji wa uchumi wa buluu,uimarishaji wa uchumi wa kidigitali, uhifadhi wa mazingira, uzalishaji wa ndani, udhibiti wa uingizaji wa bidhaa na kuimarisha miundoni ya kijamii na kiuchumi.
Meneja wa kikodi mkoa wa kaskazini Unguja, Hanii Mohommed Khamis alisema mabadiliko ya sheria ya kodi ya mwaka 2024-2025 ni hatua muhimu ya kuimarisha ulipaji kodi kwa wananchi katika misingi ya kulipa kodi kwa maendeleo ya Zanzibar.
Alisema sheria hizo zitachochea mabadiliko ya maendeleo katika Wilaya, Mikoa na Taifa Kwa ujumla, na kuwasisitiza kuendelea kulipa Kodi Kwa hiari Kwa maslahi ya nchi.
Vile vile alisema ZRA itaendelea kutoa elimu kwa wananchi ya mabadiliko ya sheria ya ulipaji kodi na kuhamasisha kulipa kodi kwa hiari ili malengo yaweze kufikiwa.
Baadhi ya washiriki wa mfunzo hayo akiwemo Mwalimu Haji Sheha na Nasra Idi Khamis waliipongeza mamlaka ya mapato ZRA kwa kuwapatia elimu ya mabadiliko ya sheria ya kodi ya nwaka 2024-2025, hatua iliyowajengea ufahamu wa mambo mapya yatakayo wasaidia katika biashara zao.
Aidha waliahidi kuwa mabalozi wazuri wa elimu hiyo kwa maendeleo ya Zanzibar.
mafunzo hayo ya siku moja yaliwashirikisha wadau wa kodi zaidi ya 50 wakiwemo wananchi na wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mkuu wa Kitengo cha habari uhusiano na huduma kwa walipakodi ZRA, Makame Khamis Moh’d, akitoa elimu ya mabadiliko ya Sheria ya kodi ya mwaka 2024-2025 Kwa wananchi na wafanyabiashara WA Mkoa wa kaskazini Unguja.
Mstahiki Meya wa baraza la Manispaa wilaya ya kaskazini ‘A’ Machano Fadhil Machano (Babla), alipokua akifungua mafunzo ya mabadiliko ya sheria za kodi 2024-2025 kwa wafanya biashara na wananchi wa mkoa wa Kaskazini Unguja
BAADHI ya wananchi na wafanyabiashara wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakifuatulia mafunzo ya mabadiliko ya sheria ya ulipaji kodi ya mwaka 2025.