Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 11.09.2024 imetoa elimu kinga juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya kwa waumini wa dini ya kikristo 310 katika Kambi ya Kisabato Sanawari 2024 jijini Arusha.
Pia waumini hao walielezewa kwa kina uhusiano wa afya ya akili na matumizi ya dawa za kulevya kwa kipindi hiki cha mwezi Septemba wa kuhamasisha na kukuza uelewa wa jamii kuhusu kuzuia watu kujiua.
Washiriki waliohudhuria kambi hiyo walihimizwa kutokuwanyanyapaa waraibu wa dawa za kulevya badala yake wawaelekeze waraibu hao katika huduma za matibabu zilizopo karibu na mazingira wanayoishi.