Na Mwandishi wetu Mpapura
Ilikuwa ni vifijo, nderemo na vigelegele kwa Wananchi kufuatia kuwashiwa umeme kwa mara ya kwanza toka Dunia iumbwe.
Wananchi hao wa Kijiji cha Mnyija kilichopo Kata ya Libobe, Tarafa ya Mpapura mkoani Mtwara wameishukuru sana Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea maendeleo ya nishati ya umeme kupitia mradi wa REA Vijijini.
“Namshukuru sana Rais Samia na uongozi wake kwa kutuletea umeme kijijini kwetu. Nakosa maneno ya kusema kwani nina furaha mno.” Alisema Mwananchi Munkarara anayeishi Mnyija.
“Afisa Tarafa Mpapura alikuja kuongea nasi tukampa kero yetu ya umeme kutokuwaka, Leo siku ya nne tunaona utekelezaji wa maombi ya kutatuliwa kero yetu, umeme umewaka. Haijapata kutokea Kiongozi kama wewe. Tunafurahi sana kututatulia changamoto ya kukosa umeme, Leo umeme umewaka Mnyija tunajionea maajabu haya kwani hatukutarajia haya kufanyika kwa Kasi na kwa muda mfupi.” Alisema Ali Abdallah mkazi wa Kijiji cha Mnyija.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnyija (CCM) Mzee Hassan Issa Chihumba amewasihi Wananchi kutunza miundombinu ya umeme.
“Hii miundombinu ya umeme tusipoilinda tutafeli. Juu ya ulinzi wa umeme upo mikononi mwetu sisi wana Mnyija. Tunashukuru sana viongozi wetu kwa kutuletea umeme, tunahaidi kuulinda umeme huu.” Alisema Mzee Chihumba, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnyija.
Kwa upande wake Afisa Tarafa Mpapura Emmanuel Shilatu aliwasihi Wananchi kuutumia umeme huo kuwaletea maendeleo yao.
“Kazi ya Serikali ni kuhakikisha inawasogezea huduma Wananchi kwa ukaribu, kama ambavyo tumewaletea na kuwasha umeme Leo hii kwa mara ya kwanza kabisa. Wananchi jukumu lenu ni kutumia umeme huu uwaletee maendeleo kwa Mtu mmoja mmoja na kwa jamii nzima. Biashara mlizokuwa mnashindwa kufanya kwa sababu ya kukosa umeme sasa fungueni. Fanyeni kazi, fanyeni biashara mjiletee maendeleo huku mkiendelea kuilinda miundombinu hii ya umeme ambayo kipekee tunamshukuru Rais Samia kwa kutoa Mabilioni ya fedha kwenye Uwekezaji wa miundombinu ya umeme nchini, ahsante sana Mhe. Rais Samia.” Alimalizia Gavana Shilatu.