KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo, akizungumza leo Septemba 11,2024 jijini Dodoma katika Mkutano wa Mtandao wa Wamiliki wa SOBA HOUSE Tanzania.
KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo,akisisitiza jambo katika Mkutano wa Mtandao wa Wamiliki wa SOBA HOUSE Tanzania.
SEHEMU ya washiriki wakisikliza hotuba ya Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo,(hayupo pichani) wakati akizungumza katika Mkutano wa Mtandao wa Wamiliki wa SOBA HOUSE Tanzania.
KAMISHNA Msaidizi wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),Dkt.Cassian Nyandindi akizungumza wakati wa Mkutano wa Mtandao wa Wamiliki wa SOBA HOUSE Tanzania.
KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mtandao wa Wamiliki wa SOBA HOUSE Tanzania.
Na.Alex Sonna-DODOMA
KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo, ametoa wito kwa watanzania kuhakikisha wanafungua vituo vya kusaidia WARAIBU wa dawa za kulevya maarufu SOBA HOUSE katika maeneo mbalimbali hasa kwenye mikoa ambayo bado haijafikiwa na huduma hiyo ili kuisaidia Serikali katika kupunguza madhara yanayotokana na matumizi ya Dawa za Kulevya.
Lyimo ametoa kauli hiyo leo Septemba 11,2024 jijini Dodoma wakati akizungumza katika Mkutano wa Mtandao wa Wamiliki wa SOBA HOUSE Tanzania.
Amesema kwa sasa kuna SOBA HOUSE 62 pekee nchini huku kukiwa na zaidi ya Waraibu wa dawa za kulevya elfu kumi na Saba hivyo bado kuna mahitaji makubwa ya SOBA HOUSE.
“Niwaombe sana wamiliki wa Soba House wahamasisheni wengine nao wafungue soba House na sio lazima mtu uwe umeshapitia katika uraibu wa dawa za kulevya ndio ufungue SOBA HOUSE kila mtu anaruhusiwa kufungua kikubwa ni kufuata taratibu na Miongozo iliyotolewa na Mamlaka,” ameeleza Lymo
Pia amewataka wamiliki wa SOBA HOUSE wasiwe wanyonge kwani Wanatoa huduma inayotambulika na Serikali na hiyo ni kazi njema kikubwa ni kuzingatia sheria na Miongozo mbalimbali iliyotolewa na Serikali katika kuwahudumia Waraibu wa Dawa za Kulevya.
“Msiwe wanyonge katika huduma hii mnayoitoa kwani ipo kisheria na serikali inatambua umuhimu wenu fanyeni kazi ya kuwahudumia watanzania kwa uhuru ila miongozo na taratibu mzingatie katika kutekeleza huduma zenu,” amesema Lyimo
Ameahidi kutoa ushirikiano kwa wamiliki wa SOBA HOUSE katika kila eneo lenye changamoto ama madhaifu ambapo yanaweza kutatuliwa na Mamlaka hiyo ikiwezekana hata kwa kutafuta wadau watakaosaidia kuzitatua.
Katika hatua nyingine amesema kazi kubwa inayofanywa na Mamlaka katika kutekeleza na kuharibu mashamba ya Bangi katika maeneo mbalimbali nchini bado haitoshi hivyo zoezi la kuwakamata watuhumiwa na kuharibu kabisa mtandao wa wauzaji na wasambazaji wa Dawa za kulevya nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Wamiliki wa SOBA HOUSE Tanzania Hamisi Shuwira amesema changamoto inayowakabili kwa sasa ni kutokuwa na Ofisi, pamoja na kutokuwa na kitambulisho maalum inayowatambulisha wao ili kuwasaidia wanapowachukua Waraibu kwa ajili ya kwenda kuwapa huduma.
“tupate vitambulisho vitakavyoonesha kazi tunayoifanya inatambulika na Serikali hata tunapowachukua Waraibu tusipate changamoto kwani Waraibu huwa wana tabia ya kubadilika badilika mwingine unaweza kumchukua alafu akaanza kusema kuwa ametekwa hivyo tukiwa na vitambulisho itatusaidia katika kazi zetu, “amesema Shiwira
Naye Katibu wa Mtandao huo Saidi Bandawe, Wakati akitoa wasilisho katika Mkutano huo ameelezea
Changamoto ya watu kufungua Soba House bila kufuata utaratibu na kusema ni vyema kufuata taratibu huku baadhi yao kutotoa taarifa za robo mwaka hivyo ni vyema kukubaliana njia gani sahihi ya kutoa taarifa.
Pia amesema suala la Kupambana na madawa ya kulevya isiwe ni kazi ya Mtandao au Mamlaka tu pia wananchi washiriki kikamilifu.
Pia amewashauri wamiliki wa Soba house kuifanya kazi hiyo kama Huduma sio Biashara hivyo ni vyema kuangalia maeneo mengine ya kufungua Soba hause sio lazima iwe Dar es Salaam au Arusha.