MKURUGENZI wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala Mhandisi Advera Mwijage,akizungumza na waandishi wa habari (hayupo pichani) leo Septemba 11,2024 jijini Dodoma kuhusu kuanza utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati safi ya kupikia hususani katika taasisi zinazohudumia zaidi ya watu 100.
MKURUGENZI wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala Mhandisi Advera Mwijage,akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 11,2024 jijini Dodoma kuhusu kuanza utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati safi ya kupikia hususani katika taasisi zinazohudumia zaidi ya watu 100.
Na Gideon Gregory, Dodoma.
KATIKA kuziwezesha kaya za Vijijini na zile zilizopo maeneo ya Vijiji-Miji kutumia nishati safi ya kupikia na zilizoboreshwa Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), inaendelea kutoa ruzuku katika uuzaji wa mitungi ya gesi ya kilo Sita yenye gesi, kichomeo na mafiga itakayouzwa katika maeneo hayo ili kumuwezesha kila mwananchi kuondokana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 11,2024 Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala Mhandisi Advera Mwijage wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza utekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia hususani katika taasisi zinazohudumia zaidi ya watu 100 na kuongeza kuwa Serikali kupitia REA imetenga bilioni 15 kwa ajili ya kuwezesha usambazaji wa majiko banifu zaidi ya 200,000.
“Tutaenda kusaini mikataba yenye thamani ya shilingi bilioni 10 ambapo makampuni manne yaliyaliyoshinda kwa ajili ya usambazaji wa mitungi hiyo ya gesi ni pamoja na Taifa Gas,Manjis,Oryx pamoja na Lake Oil.”amesema Mhandisi Advera
Amesema kuwa Jumla ya Mitungi 452,445 itasambazwa kwa bei ya ruzuku au punguzo katika mikoa yote ya Tanzania bara na kila Wilaya itanufaika na mitungi 3,255.
Aidha amesema kuwa REA imefikia makubaliano ya ushirikiano na utekelezaji wa miradi ya kujenga na kusambaza mifumo ya nishati safi ya kupikia na Jeshi la Magereza pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambapo mifumo mbalimbali ya nishati safi na iliyoboreshwa itafungwa katika taasisi hizo ili kuwezesha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika taasisi hizo.
“Kwa upande wa REA na Jeshi la magereza mikataba itakayosainiwa ina thamani ya bilioni 35.23 ambapo kati ya fedha hizo kiasi cha 75.4% sawa na bilioni 26.57 zitatolewa na REA na 24.6% sawa na bilioni 8.66 zitatolewa na magereza”amesema.
Pia amebainisha kazi zitakazofanyika kuwa ni pamoja na ujenzi wa mifumo ya bayogesi 126, usimikaji wa mifumo ya gesi ya LPG 64, usimikaji wa mfumo wa gesi asilia mmoj, usambazaji wa mitungi ya LPG ya 15kg ikiwa na jiko la plate mbili ipatayo 15,920 kwa watumishi wa magereza, usambazaji wa tani 865 za mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe kutoka STAMICO.
Mhandisi Advera amesenma utekelezaji wa miradi hiyo ya nishati safi ya na zilizoboreshwa za kupikia ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi 2024 – 2034 ambao unaelekeza ifikapo mwaka 20234 80% ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupiikia .
“Miradi hii ina lengo la kuhamasisha umma hususani taasisi zanazohudumia watu zaidi ya 100 na kaya moja moja kuacha kutumia nishati chafuzi na kutumia nishati safi zilizoboreshwa za kupikia ili kupunguza athari za kiafya, kimazingira, na mabadiriko hasi ya tabaia ya nchi”amesema.