Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Paul Maisori akitoa elimu kuhusu usalama wa miundombinu ya umeme katika kijiji cha Ishiki kata ya Iyenze Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Paul Maisori
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limefanya ziara na kutoa elimu ya umeme kwa wananchi wanaoishi katika vijiji vilivyopitiwa na Mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) awamu ya tatu mzunguko wa pili wilayani Kahama kwa kuwahamasisha wananchi kuvuta umeme kwenye nyumba zao na kulinda miundombinu ya umeme.
Ziara hiyo imefanyika leo Alhamisi Septemba 5,2024 katika Kijiji cha Ibulya na Gulla kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala na Kijiji cha Nduku kata ya Kinaga na Kijiji cha Ishiki kata ya Iyenze Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Paul Maisori amewataka wananchi kushirikiana na TANESCO kulinda miundombinu ya umeme ikiwemo Transfoma kwani miradi hiyo inatekelezwa kwa gharama kubwa.
Aidha amesema umeme ni maendeleo hivyo kuwasihi wananchi kuwa walinzi wa miundombinu ya umeme ili isihujumiwe na kusababisha wakose umeme kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
“Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan analeta fedha nyingi kwa ajili ya kufikisha umeme vijijini hakikisheni miundombinu ya umeme inalindwa usiku na mchana. Umeme ukishawaka unatakiwa uendelee kuwaka, tuwe macho tushirikiane kulinda hizi Transfoma, msizubae na kumwangalia tu mtu anapanda kwenye transfoma,hakikisheni Transfoma haiguswi, Transfoma ni mali yenu, muanze kutambuana, tumhoji yeye ni nani kwa sababu kwenye baadhi ya maeneo miundombinu inahujumiwa, mafuta yanaibiwa,Transfoma zinapigwa”,amesema Maisori.
“Pia Lindeni hizo mita, usihamishe mita ya umeme iliyopo kwenye nyumba yako na kupeleka kwenye nyumba nyingine, Hata kama mita ina jina lako hiyo ni mali ya TANESCO, ukihama iache hapo tutabadilisha jina na kama nyumba haitumiki tutachukua mita yetu na kama una nyumba nyingine basi utaomba mita nyingine na tutakupatia”,ameongeza Maisori.
Amewatahadharisha wananchi kuepuka vishoka kwa kufanya kazi na Ofisi ya TANESCO na malipo yote ya kuomba huduma ya umeme yafanywe kupitia namba ya kumbukumbu ya malipo (Control number) na kuweka mtandao wa umeme majumbani (wiring) kupitia Mkandarasi anayetambuliwa na TANESCO aliyeidhinishwa na kutambuliwa na EWURA na bodi ya Wakandarasi .
Kwa upande wake, Fundi Mchundo TANESCO wilaya ya Kahama, Denis Malewo amesema TANESCO kwa kushirikiana na REA linatekeleza mradi wa umeme vijijini ambao unawawezesha wananchi kuunganishiwa umeme kwa gharama nafuu ambapo wananchi waliopo ndani ya umbali wa mita 30 kutoka kwenye nguzo wataunganishiwa umeme kwa shilingi 27,000/= kwa umeme wa njia moja.
Fundi Mchundo TANESCO wilaya ya Kahama, Denis Malewo
Amebainisha kuwa vijiji vilivyokuwa vimepatiwa nguzo 20 vitapatiwa nguzo 40 ili kuhakikisha kuwa huduma ya umeme inawafikia wananchi wengi zaidi.
Naye Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge amesema TANESCO imeboresha huduma za umeme ambapo hakuna gharama yoyote ya kuomba umeme na mwananchi anaomba huduma ya umeme hata akiwa nyumbani bila kufika ofisi za TANESCO akitumia mfumo wa Nikonekt ambao ni mfumo rahisi wa maombi ya huduma ya umeme kwa njia ya mtandao unaotumia njia tatu ikiwemo USSD kwa kupiga *152*00#, Web portal www.tanesco.co.tz na Mobile App ya Nikonekt.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge
“Serikali inatumia fedha nyingi kuleta umeme vijijini, Mhe. Rais Dkt Samia anatumia fedha nyingi ili vijiji vipate huduma ya umeme naomba wale wote mliofikiwa na miundombinu ya umeme, vuteni umeme kwa sababu umeme ni maendeleo, umeme ni uchumi hivyo changamkieni fursa za umeme, nyumba zote zilizopo karibu na nguzo za umeme ziwe na umeme”,ameongeza Victory.
Kwa upande wake, Robert Msemo ambaye pia Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Shinyanga ametahadharisha wananchi kuepuka kukaa na kufanya shughuli chini ya transfoma ya umeme lakini pia wazazi wawalinde watoto dhidi ya umeme kwa kutoruhusu watoto kuchezea umeme.
Diwani wa kata ya Busangi Mhe. Alexander Mihayo
Diwani wa kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mhe. Alexander Mihayo na Diwani wa kata ya Iyenze Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mhe. Lucas Makulumo wamewahamasisha wananchi waliopitiwa na mradi wa umeme kuomba huduma ya umeme badala ya kuangalia tu nguzo za umeme zilizopita kwenye maeneo yao.
Nao wananchi wameishukuru TANESCO kwa kupatia elimu kuhusu huduma za umeme na kuahidi kuingiza umeme majumbani mwao na kuwa walinzi wa miundombinu ya umeme na kuepuka vishoka ambao wamekuwa wakiwatapeli kwa kuwatoza fedha za kusogeza nguzo za umeme.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Paul Maisori akitoa elimu kuhusu usalama wa miundombinu ya umeme katika kijiji cha Ishiki kata ya Iyenze Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Septemba 5,2024 . Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Paul Maisori akitoa elimu kuhusu usalama wa miundombinu ya umeme katika kijiji cha Ishiki kata ya Iyenze Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Diwani wa kata ya Iyenze Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mhe. Lucas Makulumo akizungumza wakati wa mkutano huo
Fundi Mchundo TANESCO wilaya ya Kahama, Denis Malewo akitoa elimu ya umeme katika kijiji cha Ishiki kata ya Iyenze Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Shinyanga Robert Msemo akitoa elimu ya umeme katika kijiji cha Ishiki kata ya Iyenze Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge akitoa elimu kuhusu masuala ya umeme katika Kijiji cha Nduku kata ya Kinaga Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

Fundi Mchundo TANESCO wilaya ya Kahama, Denis Malewo akitoa elimu kuhusu masuala ya umeme katika Kijiji cha Nduku kata ya Kinaga Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Mkutano ukiendelea katika Kijiji cha Nduku kata ya Kinaga Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Mkazi wa Kijiji cha Nduku kata ya Kinaga Halmashauri ya Manispaa ya Kahama akisoma kipeperushi cha namna ya kupata huduma ya huduma
Wakazi wa Kijiji cha Nduku kata ya Kinaga Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wakisoma vipeperushi vya namna ya kupata huduma ya huduma
Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Paul Maisori akitoa elimu kuhusu usalama wa miundombinu ya umeme katika Kijiji cha Ibulya kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala

Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge akitoa elimu kuhusu masuala ya umeme katika Kijiji cha Ibulya kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala

Mkazi wa Kijiji cha Ibulya kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala akiuliza swali
Mkazi wa Kijiji cha Ibulya kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala akiuliza swali
Mkazi wa Kijiji cha Ibulya kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala akisoma kipeperushi
Wakazi wa Kijiji cha Ibulya kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala wakiwa kwenye mkutano
Wakazi wa Kijiji cha Ibulya kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala wakiwa kwenye mkutano
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Shinyanga Robert Msemo akigawa vipeperushi kwa Wakazi wa Kijiji cha Ibulya kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala

Fundi Mchundo TANESCO wilaya ya Kahama, Denis Malewo akitoa elimu kuhusu masuala ya umeme katika kijiji cha Gulla kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Shinyanga Robert Msemo akitoa elimu kuhusu masuala ya umeme katika kijiji cha Gulla kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Paul Maisori akitoa elimu kuhusu masuala ya umeme katika kijiji cha Gulla kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
Wakazi wa kijiji cha Gulla kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala wakiwa kwenye mkutano
Mkazi wa kijiji cha Gulla kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala akiuliza swali

Mkazi wa kijiji cha Gulla kata ya Busangi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala akisoma kipeperushi..
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog