Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Asasi ya Youth and Community Rehabilitation (YCR) tarehe 28.08.2024 imetoa elimu ya kupiga vita dawa za kulevya pamoja na kuelezea madhara ya tatizo la dawa za kulevya katika Shule ya Msingi ya Margaret England Burks iliyopo Kata ya Ngaramtoni Arumeru (W) Arusha (M).
Elimu hiyo ilitolewa kwa wanafunzi zaidi ya 200 ambapo mbali ya kuwapa elimu kinga dhidi ya tatizo la dawa za kulevya lakini pia walipewa mbinu wanazopaswa kuzitumia ili kujiepusha na dawa hizo.
Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini itaendelea kushirikiana na Asasi za kiraia katika utekelezaji wa majukumu yake kwa lengo la kuwawezesha na kuimarisha mashirikiano ambayo yatasaidia kueneza elimu sahihi kwa jamii ili iweze kupata matokeo yenye tija katika eneo la uelimishaji na huduma za ustawi wa jamii.