Na Prisca Libaga Tanga
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Asasi za Gift of Hope Foundation, Tanga Drug Free Organization pamoja na Organization of Youth Against Risk Behaviors (OYARB) tarehe 27.08.2024 imetoa elimu kinga dhidi ya dawa za kulevya kwa Umma kupitia Redio ya Kijamii ya Maarifa 105.03MHZ pamoja na wanafunzi kutoka katika Shule tatu za Sekondari zilizopo Tanga Mjini.
Wanafunzi 1,119 Shule ya Sekondari ya Maweni, 450 kutoka Shule ya Sekondari Ummy Mwalimu na 785 kutoka Shule ya Sekondari Pongwe zote za jijini Tanga waliweza kupatiwa elimu hiyo.
Ofisi ya DCEA Kanda ya Kaskazini itaendelea kuihamasisha jamii ishirikiane na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutowanyanyapaa waraibu wa dawa hizo badala yake wawaelekeze katika huduma za matibabu zilizopo karibu na mazingira yao wanayoishi.