Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameapa kiapo cha uaminifu bungeni leo Agosti 27, 2024.
Hamza Johari ameapa mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge.
Hamza aliteuliwa na Rais, Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Agosti 14, 2024 akichukua nafasi ya Jaji Eliezer Feleshi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Mwanasheria Mkuu ndiye mshauri mkuu wa kisheria wa Serikali na Bunge akiwa na jukumu la kusimamia masuala ya kisheria.
kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Hamza Johari alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCCA).