Na Rahma Khamis Maelezo
Barazan la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) limewataka waalimu wa kiswahili wanaosomesha wageni kuzitumia fursa za kimasomo zinazotokea ili kuendelea kuieneza lugha hiyo.
Akifungua Mafunzo kwa waalimu hao katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dokt Mwanahija Ali Juma amesema lugha ya kiswahili ni lugha ya taifa ambayo kwa Sasa ni bidhaa kwa wageni hivyo Mafunzo hayo yatawezesha kuendelea kuitangaza Ulimwenguni kote.
Amesema kiswahili kimekua kikitumiwa na wageni weni wanaofika nchini hivyo fursa hiyo itasaidia kuingiza Pato kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Aidha Dkt Mwanahija amewanasihi watanzania kuendelea kutumia kiswahili ili iwe ni fursa kwa wengine.
Mapema akizungumza katika Mafunzo hayo Mratibu wa Mafunzo ya kiswahili kwa wageni bi Daulat Abdullah Said amesema Mafunzo hayo yameanza kutolewa Toka mwaka 2022 na Hadi Sasa zaidi ya wahitinu 200 washapatiwa taaluma hiyo Unguja na Pemba.,
Wakitoa mbinu za ufundishaji wageni kwa waalimu hao Mkufunzi Dkt. Shani Suleiman Khamis na Dkt Kijakazi Omar Makame kutoka SUZA wawamefahamisha kuwa walimu wanaofundisha wageni lazima wajue sarufi ya lugha kwani bila Kufahamu sarufi huwezi kufundishia wageni hao.
Nao wanafunzi waliopatiwa Mafunzo hayo wamesema kuwa wameamua kuisomesha lugha hiyo kwa wageni ili kujipatia kipato.
Aidha wamewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kufundishia lugha hiyo kwani ni ambayo na haina ugumu na kila mtu anaweza kuifahamu.
Hata hivyo wameiomba Serikali kuandaa waalimu wa kufundishia lugha hiyo ili kupata waalimu wazuri watakaoweza kufundisha wageni .
Mafunzo hayo yameandaliwa na Baraza la Kiswahili BAKIZA na limewashikisha walimu mbalimbali Tanzania.