Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Sima Cosintantine akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kilicholenga kujadilili utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Jiji la Mwanza
Baadhi ya washiriki wa kikao wakiwa ukumbini
Picha ya pamoja
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wadau mbalimbali wa maendeleo Mkoani Mwanza wamekutana kujadili utekelezaji wa mpango kabambe (Master Plan) wa Jiji hilo wa mwaka 2015 -2035
Mpango huo ulizinduliwa mwaka 2019 kama Dira ya miaka 20 ya kusimamia Maendeleo ya Jiji ikiwemo kutoa muongozo wa kuboresha na kuendeleza matumizi ya ardhi, miundombinu, mawasiliano pamoja na uhifadhi wa mazingira.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Sima Constantine, amesema wadau wamekutana kufanya mapitio ya utekelezaji wa mpango huo ili kutathimini,kuboresha ustawi na ustahimilivu wa Jiji hilo.
“Mpango huu umejikita katika maboresho na uendelezaji wa miradi mbalimbali katika kuibua uchumi,upatikanaji wa huduma za kijamii kama vile ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambao utasaidia katika usafirishaji wa bidhaa ndani na nje ya nchi,upanuzi wa uwanja wa ndege,uendelezaji wa makazi yasiyo rasmi mfano maeneo ya Igogo,Pamba na Mabatini,
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Butimba Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji Marwa Mbusiro amewaomba wananchi kuachana na ujenzi holela unaweza kuwasababishia hasara badala yake wafate sheria na taratibu kwakufika kwenye taasisi husika ili waweze kupewa vibali vya ujenzi.
“Ili Jiji la Mwanza lizidi kupendeza ni lazima tujenge kwakufuata utaratibu wa ujenzi ambao upo kwenye Mpango Kabambe wa Jiji la Mwanza, kuna baadhi ya watu wachache wanaohujumu Mpango huu kwa maslahi yao binafsi kwakutoa vibali vya ujenzi hata sehemu ambazo hazistahili kuwa makazi ya watu hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini wanapokuwa wanafatilia vibali vya ujenzi”, amesema Mbusiro
Naye Afisa Mipango Miji Mwandamizi wa Jiji la Mwanza Evodia Paul, amesema wamepiga hatua katika baadhi ya sekta kwa asilimia 35 katika utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Jiji ambapo ameeleza kuwa ifikapo mwaka 2035 watakuwa wamekamilisha katika sekta zote.
“Huu mpango Kabambe unaelekeza kwakipindi fulani nini kifanyike na endapo tutakuwa na sehemu ambayo hatujaitekeleza huwa tunahuisha ili yale mambo ambayo yanakuwa hayajafanyika yaweze kufanyika, hata sasa hivi tumehuisha mpango wa 2002 -2012 ndio ambao tunaendelea nao na tumeuboresha kutokana na kasi ya ukuaji wa dunia inayohitaji miji ya kisasa zaidi”, amesema