WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa,akizungumza wakati akitoa tangazo la uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 lililoambatana na uzinduzi wa nembo itakayatumika kwenye uchaguzi pamoja na utolewaji wa muongozo wa uchaguzi huo,hafla iliyofanyika leo Agosti 15,2024 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Ndg. Juma Ali Khatibu,akizungumza wakati wa kutangazwa kwa tangazo la uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 lililoambatana na uzinduzi wa nembo itakayatumika kwenye uchaguzi pamoja na utolewaji wa muongozo wa uchaguzi huo,hafla iliyofanyika leo Agosti 15,2024 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa Mhe.Martin Shigella,akizungumza wakatiwa kutangazwa kwa tangazo la uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 lililoambatana na uzinduzi wa nembo itakayatumika kwenye uchaguzi pamoja na utolewaji wa muongozo wa uchaguzi huo,hafla iliyofanyika leo Agosti 15,2024 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) ,akizungumza wakati akitoa tangazo la uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 lililoambatana na uzinduzi wa nembo itakayatumika kwenye uchaguzi pamoja na utolewaji wa muongozo wa uchaguzi huo,hafla iliyofanyika leo Agosti 15,2024 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa,akizindua nembo itakayatumika kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 ,hafla iliyofanyika leo Agosti 15,2024 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa tangazo la uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 lililoambatana na uzinduzi wa nembo itakayatumika kwenye uchaguzi pamoja na utolewaji wa muongozo wa uchaguzi huo,hafla iliyofanyika leo Agosti 15,2024 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imetangaza Novemba 27 mwaka huu kuwa siku rasmi ambayo uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika na Upigaji wa kura utaanza saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa kumi kamili jioni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohammed Mchengerwa,ametangaza tarehe rasmi ya uchaguzi huo leo Agosti 15,2024 jijini Dodoma, mbele ya viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa na wadau wengine wa maendeleo.
“Nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huu ni Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka za Wilaya.Kwa nafasi hizo,uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za Mwaka
2024 (Tangazo la Serikali Na. 571 la Mwaka 2024), nyingine ni Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo.
Kwa nafasi hiyo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na. 572 la Mwaka 2024),
Nakuongeza kuwa “nafasi nyingine ni Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka za Miji.
Kwa nafasi hizo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na.573 la Mwaka 2024) na Mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi Mchanganyiko la Wanaume na Wanawake) na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi la Wanawake) katika Mamlaka za Miji.
Kwa nafasi hizo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka za Miji za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na. 574 la Mwaka 2024), ” ameeleza Mchengerwa
Aidha, katika hatua nyingine Mchengerwa amezitaka Taasisi zinazotaka kutoa elimu ya mpiga kura kufanya maombi maalumu kupitia kwa Katibu Mkuu wa ofisi ya Rais TAMISEMI ili wapate kibali cha kutoa elimu hiyo kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Ndg. Juma Ali Khatibu amesema wao kama Baraza la Vyama vya Siasa hawategemei kuona migogoro baada ya Uchaguzi kwani kuna maisha mengine yataendelea baada ya Uchaguzi.
Pia ametoa wito kwa watendaji wa TAMISEMI watakaohusika katika usimamizi wa mchakato wa uchaguzi huo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa haki na weledi na kuzingatia Taaluma zao na misingi ya Haki ili kutimiza zile 4R za Rais Samia.
Naye Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa Martin Shigella amesema ushiriki wa Viongozi wa vyama vya siasa katika mchakato wa leo unakwenda kuongeza hari na hamasa kwa wananchi kushiriki katika uchaguzi huo.
“Hata sisi kule mikoani tuna viongozi wa vyama vya siasa na tunashirikiana nao Sana katika kuhakikisha uchaguzi huu una kuwa wa haki na uhuru ili kuhakikisha wanapatikana viongozi bora ambao watatanguliza maslahi ya Taifa mbele,” ameeleza Shigella
Kampeni za UCHAGUZI wa serikali za mitaa 2024 zitafanyika siku saba kabla ya siku ya uchaguzi. Aidha, Kanuni zinaelekeza, kila Chama cha Siasa kinachoshiriki uchaguzi kitawasilisha ratiba yake ya mikutano ya kampeni ya uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi si chini ya siku saba kabla ya kuanza kwa kampeni.