Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri, amesema Wizara ya Maji imeandaa mafunzo ya siku mbili katika kuhakikisha usalama wa mabwawa ya maji na tope sumu unaimarishwa.
Amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwa kushirikiana na TanzaniabChamber of Mines na yatafanyika mkoani Mwanza .
Amesema hayo katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Maji uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
Ameongeza kuwa mafunzo yatahusisha watalaam kutoka wamiliki wa migodi kwa ajili ya usalama wa mabwawa ya tope sumu, wamiliki wa mabwawa makubwa ya maji, wataalam wa mabwawa waliosajiliwa na wataalam kutoka Serikalini.
Wizara ya Maji kupitia Idara ya Rasilimali za Maji ina jukumu la kuhakikisha mabwawa ya maji na tope sumu yanakidhi vigezo vya usalama wa mabwawa kwa mujibu wa Sheria ya Rasilimali za Maji Na. 11 ya Mwaka 2009 na maboresho yake Na. 8 ya Mwaka 2022. Pamoja na kanuni za usalama wa mabwawa GN 237 za mwaka 2013 na mabresho yake GN 55 ya mwaka 2020.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali za maji wizara ya Maji Dk. George Lugomela, amesema kuwa wao kama wasimamizi wa rasilimali za maji nchini wamekuwa watoa elimu kuhusu umuhimu wa uzinagiaji wa sheria, miongozo na kanuni za uchimbaji mabwawa ya maji na yale ya kuhifadhia tope sumu.
Naye Mwenyekti wa TCM, Mhandisi Philbert Rweyemamu, amesema kuwa mafunzo hayo ni mwendeleo wa yale yaliyofanyika mwaka jana ambayo yalihusisha uwekaji wa vifaa vya kufuatilia mwendendo wa usalama wa mabwawa.
“Mafunzo hayo yaliandaliwa na TCM kwa kushirikiana na Wizara ya Maji na yalijenga uelewa na kuongeza ufanisi kwa washiriki kutokana na kubadilishana ujuzi kutoka kwa wataalamu na mataifa yaliyoendelea kwenye eneo linalohusu usalama wa mabwawa hali hiyo iliwezesha kuwekwa maazimio, mojawapo likiwa ni kufanya mafunzo kama hayo kwa kila mwaka,”amesema