WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Ridhiwani Kikwete,akizindua Sera ya Taifa ya vijana ya mwaka 2007 kwa ajili ya kuwasaidia kutatua changamoto zao.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imezindua Sera mpya ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 toleo la 2024, ambayo inakwenda kujibu changamoto mbalimbali za vijana na kutoa mwongozo wa kuanzishwa rasmi kwa Baraza la Taifa la Vijana.
Hayo yamebainishwa leo Agosti 12,2024 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu,Mhe. Ridiwani Kikwete, wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa.
“Serikali imekwisha kamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Vijana ya mwaka 2007 na marekebisho yake imefanyiwa mwaka 2024 na leo hii tunakwenda kuizindua muda mfupi ujao.
“Ndugu washiriki changamoto nyingi zinazoelezwa kwa vijana zinatokana na ukweli kwamba yako baadhi ya maeneo hayana miongozo yake kupitia sera hii ya vijana ambayo tutaizundua leo nina hakika kabisa vilio vya vijana wengi vinakwenda kupataiwa ufumbuzi baada ya kupitishwa kwa sera hii”ameeleza
Aidha, amesema kuwa sera hiyo inaeleza uelekeo na njia ambazo wanakwenda kuzitumia kwa pamoja ili kufikia malengo ambayo yanatatua matatizo waliyonayo vijana.
“Sera hii inakwenda kuanzisha baraza la taifa la vijana uanzishaji wa baraza hili la vijana unakwenda kuwa muarobani wa kutambua na kutatua changamoto nyingi za vijana.
“Vijana wamekosa maeneo ya kueleza changamoto zao vijana walikosa watu wa kuwasikiliza, vijana walikosa msukumo wa kufikisha changamoto zao na kuzitafutia majawabu kwa pamoja”amesema Mhe.Ridhiwan
Amesema, ujio wa sera hiyo ya vijana na uudwaji wa baraza la taifa la vijana unaonesha wazi azma ya Rais Samia kujidhatiti na changamoto zote zinazo wakabili vijana zinapatiwa majibu.
Hata hivyo amesema kuwa sera hiyo pia inakwenda kutambua vijana katika sekta zote wanaofanya kazi katika maeneo hatarishi ikiwemo ya madini, maeneo ya uzalishaji mali ikiwemo mashambani na kwenye mifugo.
“Wapo vijana wanaofanya kazi za sanaa ikiwemo wabunifu, muziki, michezo, ubunifu na utungaji wa sanaa mbalimbali sera hii inakwenda katika maeneo hayo.
Pia ametoa wito kwa maafisa kazi kutambua kuwa nafasi zao siyo za kukaa ofisini wakisubiri vijana waje kulia na kueleza changamoto zao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga,amesema katika kuadhimisha siku ya vijana, wameendesha kongamano la siku mbili lililokutanisha vijana zaidi ya 3,000 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga,akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa iliyoongozwa na kauli mbiu inayosema “Vijana na matumizi ya fursa za kidigitali kwa maendeleo endelevu yaliyoambatana na uzinduzi wa sera ya Taifa ya vijana ya mwaka 2007 kwa ajili ya kuwasaidia kutatua changamoto zao,yaliyofanyika leo Agosti 12,2024 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa iliyoongozwa na kauli mbiu inayosema “Vijana na matumizi ya fursa za kidigitali kwa maendeleo endelevu yaliyoambatana na uzinduzi wa sera ya Taifa ya vijana ya mwaka 2007 kwa ajili ya kuwasaidia kutatua changamoto zao,yaliyofanyika leo Agosti 12,2024 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Vijana, Charles Ruben,akizungumza kwa niaba ya Vijana kwenye Maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa iliyoongozwa na kauli mbiu inayosema “Vijana na matumizi ya fursa za kidigitali kwa maendeleo endelevu yaliyoambatana na uzinduzi wa sera ya Taifa ya vijana ya mwaka 2007 kwa ajili ya kuwasaidia kutatua changamoto zao,yaliyofanyika leo Agosti 12,2024 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kwenye Maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa iliyoongozwa na kauli mbiu inayosema “Vijana na matumizi ya fursa za kidigitali kwa maendeleo endelevu yaliyoambatana na uzinduzi wa sera ya Taifa ya vijana ya mwaka 2007 kwa ajili ya kuwasaidia kutatua changamoto zao.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Ridhiwani Kikwete,akizindua Sera ya Taifa ya vijana ya mwaka 2007 kwa ajili ya kuwasaidia kutatua changamoto zao.