Na Prisca Libaga Arusha
MAAFISA Tarafa na Watendaji wa kata Mkoa wa Arusha, wamekumbushwa umuhimu wao wa kutunza Siri za Serikali na ofisi zao ili kutokuleta migogoro na kuhatatisha maisha ya baadhi ya watumishi pindi kunapochukuliea hatua zinazowaumiza.
Hayo yameelezwa Augosti 8 na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Mussa Albano Misaile, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji na utatuzi wa migogoro Maafisa hao yanayofanyika kwenye Ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha
Amesema wapo baadhi ya Maafisa hao wamekuwa wakitoa siri za Serikali na huko ni kufanya kinyume na maadili ya utumishi wa umma na akasisitiza utunzaji wa siri za Serikali Ili kuondoa migogoro
Misaile amesema mafunzo hayo yanawasaidia kuwapa mwongozo na kuwawezesha kuwa wabunifu na kuzitatua changamoto za kimaadili na uzalendo kwa kuwa Utumishi una changamoto kubwa sana pindi zinapojitokeza .
Amesema baadhi ya watumishi ni wapya hivyo mafunzo hayo yatawaeezesha kufahamu mipaka na majukumu yao na wao ni viungo kati yao serikali na wadau na wananchi .
Amewataka watendaji wa kata,(WEO ) wanapopanga mipango ya maendeleo lazima wawashirikishe Maafisa tarafa ili wawe na uelewa wa pamoja kutatua kero na changamoto na kuelewa kinachotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao.
Akawataka wawe na uwezo wa kutafisiri taarifa mbalimbali zikiwemo Sheria na Sera sanjari na kutoa ushauri sahihi kwa Wakurugenzi wa halmashauri na hivyo kero na changamoto zitatuliwe kwa wakati bila kusubiri mkuu wa Wilaya au Viongozi wa juu zaidi
Amesema kwenye maeneo yao kuna changamoto nyingine ikiwemo migogoro ya ardhi ,migogoro ya wao kwa wao,migogoro na wanasiasa ,wapo baadhi wanashindwa kutatua migogoro kutokana na kutokuwa na uelewa wa masuala ya Sheria na Sera .
Awali Mkurugenzi msaidizi Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais ,Ibrahim Minja, amesema TAMISEMI imeandaa mafunzo hayo kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa wa masuala mbalimbali ya kiutendaji kupitia Programu ya uimarishaji mikoa kupitia Serikali za mitaa.
Amesema kufuatia mafanikio yaliyopatikana kupitia awamu ya kwanza na ya pili Programu hiyo Serikali ilianzisha mafunzo hayo kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa tarafa na watendaji wa kata zote Nchini ili kuongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuwahudumia wananchi.
Minja,amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu tano na tayari mikoa 20 imeshapata mafunzo hayo ambayo mara baada ya Arusha wanaenda Kilimanjaro na kuhitimisha mafunzo hayo mkoani Tanga wiki ijayo na hivyo watakuwa wamefikia malengo ya kutoa mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yanatokewa na wakufunzi wabobezi kutoka Chuo Cha Serikali za mitaa,cha Hombolo mkoani Dodoma kwa pamoja na Chuo cha Utumishi wa umma .