Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mhe Almishi Issa Hazali,akimpongeza Kamanda oparesheni Kanali Sadicky Mihayo,kwa usimamizi mzuri wa mradi wa nyumba 73 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya tope yalitokea Disemba mwaka jana zilizojengwa na Kampuni ya SUMA JKT mara baada ya hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba hizo 73 na SUMA JKT.
Na.Alex Sonna-HANANG,MANYARA
HALMASHAURI ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara,imeipongeza Kampuni ya SUMA JKT kwa kukamilisha kwa wakati na katika ubora mkubwa ujenzi wa nyumba 73 kwa ajili wa waathirika wa mafuriko ya tope yalitokea Disemba mwaka jana.
Katika mafuriko hayo ambayo yalisababisha vifo vya baadhi ya watu na kuharibu miundombinu ya barabara na kuwacha wakazi wengi wa eneo hilo bila makazi.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mhe Almishi Issa Hazali ,alibainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba hizo 73 za waathirika wa mafuriko ya tope yaliyotea Disemba mwaka jana.
Alisema, wanaishuru SUMA JKT, kwa kufanikisha ujenzi wa nyumba hizo 73 kwa wakati na kwa ubora hali ambayo itakwenda kujibu changamoto ya baadhi ya wakazi wa eneo hilo kupata makazi baada ya mafuriko hayo.
“Tunayofuraha kupokea nyumba hizi tunamshuru sana Rais Samia Suluhu Hassan, Disemba mwaka jana mafuriko ya tope yaliikumba wilaya yetu na hali ilikuwa mbaya sana miundombinu iliharibika, soko na makazi pia yalisombwa na mafuriko na kuacha baadhi ya watu bila makazi ya kuishi.
“Rais alifanya kazi nzuri kuhakikisha kuwa hali inarudi sawa na leo hii tumepokea nyumba 73 ambazo serikali ilitoa fedha kwa ajili ya kuwajengea waathirika na leo hii tunakabidhiwa tunawashuru sana SUMA JKT kwa kufanikisha jambo hili kwa wakati na kwa ubora zaidi”alisema
Kwa upande wake Kamanda oparesheni Kanali Sadicky Mihayo, alisema ujenzi nyumba hizo 73 ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan na wakuu wake walioagiza SUMA JKT kusimamia utekelezaji wa mradi huo.
“Nyumba hizi 73 ni kwa ajili ya watu walioathirika na mafuriko ya tope yaliyoikumba wilaya hii mwaka jana leo hii tumekabidhi nyumba hizi ambazo kila moja ina vyumba vitatu, sebure na nje lipo jiko na choo”alisema
Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mhe Almishi Issa Hazali,akiwa na Kamanda oparesheni Kanali Sadicky Mihayo,wakikagua mradi wa nyumba 73 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya tope yalitokea Disemba mwaka jana zilizojengwa na Kampuni ya SUMA JKT mara baada ya hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba hizo 73 na SUMA JKT.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mhe Almishi Issa Hazali,akiwa na Kamanda oparesheni Kanali Sadicky Mihayo,wakikagua mradi wa nyumba 73 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya tope yalitokea Disemba mwaka jana zilizojengwa na Kampuni ya SUMA JKT mara baada ya hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba hizo 73 na SUMA JKT.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mhe Almishi Issa Hazali,akimpongeza Kamanda oparesheni Kanali Sadicky Mihayo,kwa usimamizi mzuri wa mradi wa nyumba 73 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya tope yalitokea Disemba mwaka jana zilizojengwa na Kampuni ya SUMA JKT mara baada ya hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba hizo 73 na SUMA JKT.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mhe Almishi Issa Hazali,akiwa na Kamanda Oparesheni Kanali Sadicky Mihayo,akionyesha muonekano wa Nyumba zinazojengwa kwa ajili ya waathirika wa maafa ya maporomoko ya Tope Warret-Gidagamowd Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mhe Almishi Issa Hazali,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa Nyumba 73 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya tope yalitokea Disemba mwaka jana zilizojengwa na Kampuni ya SUMA JKT hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba hizo ilifanyika katika kijiji cha Warret-Gidagamowd Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Kamanda Oparesheni Kanali Sadicky Mihayo,akielezea jinsi walivyofanikisha ujenzi huo kwa muda mfupi nyumba 73 kwa ajili ya waathirika wa maafa ya maporomoko ya Tope zilizopo Warret-Gidagamowd Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Msaidizi wa Operesheni Kamanda Luteni Kanali Ashrafu Hassan,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Nyumba 73 kukabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Ujenzi SUMAJKT Mhandisi Morgan Nyonyi,akielezea ubora na uimara wa Nyumba 73 zilizojengwa na SUMAJKT kwa ajili ya waathirika wa maafa ya maporomoko ya Tope zilizopo Warret-Gidagamowd Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Muonekano wa Mradi wa Nyumba 73 zilizojengwa SUMA JKT kwa ubora Mkubwa na muonekano mzuri kwa ajili ya waathirika wa maafa ya maporomoko ya Tope zilizopo Warret-Gidagamowd Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.