Afisa Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Bw. Msafiri Mkunda (wa kwanza kulia), akimuelezea Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (wa pili kulia), kuhusu aina na upandaji majani ya Lukina kwa ajili ya malisho ya Mifugo, mara baada ya kuwasili katika maeneo ya vipando, ni katika Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
……
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, amehimiza matumizi ya teknolojia ya Mifugo na Uvuvi kwa wafugaji ili kuweza kuleta tija katika uzalishaji.
Akizungumza, leo Agosti 2, 2024 mkoani Dodoma alipotembelea kwenye Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa mkoani Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Shemdoe amesema kuwa katika haya maonyesho kuna teknolojia nzuri sana ya ufugaji na uvuvi kwa hiyo wafugaji na wavuvi wote waje kuchukua teknolojia hii ili kuboresha mifugo yao.
“mnakumbuka Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa jana alisema maana halisi ya haya maonesho ni kwamba wakulima waje kuchukua teknolojia” amesema Prof. Shemdoe
Aidha, Prof. Shemdoe alisema haya maonesho ya nanenane ni kwa mara ya kwanza yanaadhimishwa kimataifa hapa mkoani Dodoma na ameweza kutembelea mabanda mbalimbali ya mifugo na uvuvi pamoja na kilimo ikiwa na sehemu ya vipando.
Vilevile Prof. Shemdoe ametoa wito kwa watanzani kutumia siku nane kutembelea maonesho haya ya nanenane ili kujionea teknolojia mbalimbali zinazopatikana katika maonesho haya ambazo zitawasaidia katika shughuli za uzalishaji.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri, amemshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kutembelea maonesho hayo ya nanenane.
Vilevile Mhe. Jabir amesema, maonesho haya yatawasaidia wananchi wa Tanzania kubadirisha maisha yao kwa kuongeza kipato na kukuza uchimi wa nchi, kwani elimu wanayoipata kwenye maonesho haya yatakuwa na maboresho na mapinduzi makubwa kwao.
*Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, akitazama mifugo kwenye Banda la Kampuni ya Maziwa ya ASAS, mara baada ya kutembelea eneo hilo, ni katika Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
*Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (wa kwanza kushoto), akionyeshwa Samaki aina ya Bunju baada ya kuelezewa sifa zake na Afisa Masoko wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania, Bi. Halima Tosiri (wa kwanza kulia), mara baada ya kutembelea mabanda ya wadau mbalimbali na Taasisi/Idara/Vitengo vilivyopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ni katika Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
*Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (wa kwanza kulia), akimsikiliza moja ya Vijana waliohitimu Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (Build Better Tomorrow – BBT), Bi. Resti Mgonja (wa kwanza kushoto), akielezea kuhusu mikataba waliopewa na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ya kupangishwa vitalu vyenye ukubwa wa hekari 10 kwa kila kijana wa BBT kwa kipindi cha miaka mitano bure ili wakafuge kibiashara, ni katika Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
*Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Wanyama, Dkt. Asimwe Rwiguza (wa nne kulia), akimuelezea Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (wa kwanza kushoto), Mpango wa mabadiliko wa Sekta ya Mifugo ambao umejikita katika maeneo saba ya kipaumbele, baada ya kuwasili katika Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ni katika Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
*Afisa Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Bw. Msafiri Mkunda (wa kwanza kulia), akimuelezea Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (wa pili kulia), kuhusu aina na upandaji majani ya Lukina kwa ajili ya malisho ya Mifugo, mara baada ya kuwasili katika maeneo ya vipando, ni katika Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.