Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Uwakala wa vyuo vikuu nje ya nchi ya Global Education link Ltd , Abdulmalik Molllel akizungumza kuhusu Maonesho hayo.
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Uwakala wa vyuo vikuu nje ya nchi ya Global Education link Ltd , Abdulmalik Molllel aliyeko kushoto akitoa maelezo kwa mmoja wa wanafunzi waliofika kwenye Maonesho hayo kwa ajili ya kupata maelezo namna ya kujiunga na chuo nje ya nchi.
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha.Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za kielimu zilipo nje ya nchi ili kukuza uchumi wa Tanzania kupitia teknolojia zinazotumika katika nchi za nje.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Uwakala wa vyuo vikuu nje ya nchi ya Global Education link Ltd , Abdulmalik Molllel wakati akizungumza katika maonesho ya vyuo vikuu nje ya nchi yaliyofanyika mkoani Arusha.
Aidha maonesho hayo yalizishirikisha vyuo vikuu 15 kutoka nje ya nchi ambapo lengo kubwa ni kuweza kuwajulisha wanafunzi wa Tanzania kuwa kuna fursa za elimu zilizopo nje ya nchi na kuweza kuwaunganisha moja kwa moja na vyuo vya nje ya nje kwa wale wanahitajika huduma hiyo.
Mollel amesema kuwa, watanzania wengi ambao wanahitaji kusoma nje ya nchi ila changamoto wengi hawajui pa kuanzia ambapo amewataka kuitumia Taasisi hiyo ili kuweza kujiunga na vyuo vilivyopo nje ya nchi kulingana na kozi zote wanazohitaji.
“Wanafunzi wetu wanapopa fursa ya kwenda kusoma nje ya nchi wanapata mwanya mzuri wa kwenda kutangaza fursa zilizopo nchini Tanzania ikiwemo utalii mbalimbali na hatimaye kuweza kukuza uchumi wa Tanzania Tanzania kupata wawekezaji bora kwa maisha ya baadaye.”amesema Mollel.
Mollel amefafanua kuwa, wanafunzi wetu wanapoenda kusoma nje ya nchi itawasaidia wao kujifunza zaidi ujuzi na teknolojia zilizopo kule na kuweza kuleta ujuzi huo hapa nchi na kuweza kuwa na vijana wazuri waliobobea katika maswala mbalimbali na kuweza kuwa mabalozi wazuri kwa wengine .
Aidha amesema kuwa, kupitia Taasisi hiyo wanawaandaa vijana kutegemea ajira ya duniani na nvijana wataweza kuonana na vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo nje ya nchi na kupata maelezo kulingana na uhitaji wao na kuweza kusajiliwa rasmi kwa wale waliopo tayari .
“Pia tunatoa ufadhili wa asilimia 100 kwa wanafunzi hapa hapa kulingana na matokeo yake na kama kweli anakidhi nafasi ya kusoma vyuo vikuu nje ya nchi kwani kupitia chuo hiki wanafunzi wengi sana wanapata ufadhili .”amesema Mollel.
Amesema kuwa wao wana jukumu kubwa la kuhamasisha watanzania kutambua fursa zilizopo katika vyuo vikuu vya nje ya nchi ambapo amewataka wakuu wa shule mbalimbali kuhamasisha wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne na sita kukitumia chuo hicho kuweza kupata fursa ya kusoma nje ya nchi.
“Unajua mwanafunzi wanapoenda kusoma nje ya nchi wanapata fursa ya kujifunza maswala mengi ya kule na wanaporudi Tanzania wanakuwa wawekezaji wazuri waliobobea katika maswala mbalimbali na hatimaye kuja kuwa wawekezaji wazuri na kuanzisha viwanda mbalimbali.na kuweza kuwafundisha na vijana wengine ujuzi walioupata kule.
Aidha Mollel ameongeza swala la kuratibu kila kitu hadi kuhakikisha mwanafunzi umefanikiwa kwenda nje ya nchi ni la Taaasisi hiyo hivyo kuwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo kwani Taasisi hiyo imewarahisishia kazi kwa kiwango kikubwa sana .
Naye Mmoja wa wanafunzi waliofika katika maonesho hayo ,Alice Porokwa amesema kuwa kitendo cha Taasisi hiyo kuwaletea huduma hiyo hapa karibu kumesaidia sana kwani alikuwa anatamani kwenda kusoma nje ya nchi ila alikuwa hajui pa kuanzia ila kupitia Taasisi hiyo ameweza kupata uelewa na kukutana na vyuo hivyo moja kwa moja .
“Nilikuwa sijui kama naweza kumudu kusoma nje ya nchi kwani nilijua ni gharama kubwa sana lakini nimefika hapa baada ya kuona vyuo vilivyopo nchi mbalimbali kumbe unaweza kusoma hadi kwa shs milioni 2,3 hadi tano kwa mwaka kulingana na kozi unayohitaji na hii wengi watamudu kwani hizo ni ada za shule binafsi katika elimu ya msingi hivyo nawaomba wazazi wachangamkie hizo fursa na kuleta watoto kusoma nje ya nchi kwa kiwango kikubwa sana .”amesema.