NAIBU Wanasheria Mkuu wa Serikali balozi Prof. Kennedy Gastorn, aakizungumza Leo Julai 31,2024 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi baina ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wakurugenzi wa divisheni na wakuu wa vitengo vya sheria kutoka taasisi mbalimbali za serikali.
Na.Alex Sonna_DODOMA
NAIBU Wanasheria Mkuu wa Serikali balozi Prof. Kennedy Gastorn amewataka mawakili wa serikali kutekeleza falsafa ya Ofisi ya Mwansheria mkuu wa serikali ya kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na ubora.
Prof. Gastorn, ameyasema hayo Leo Julai 31,2024 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi baina ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wakurugenzi wa divisheni na wakuu wa vitengo vya sheria kutoka taasisi mbalimbali za serikali.
Amesema mawakili wa serikali wanao wajibu wa kuteleza majukumu yao kwa weledi na ubora na kushirikiana na vyombo vingine kusaidia wanachi.
” Falsafa ya Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ni kuteleza majukumu yetu kwa kuzingatia weledi na ubora kujitambua na kuteleza wajibu wetu
Aidha, akizungumzia kuhusu kikao kazi hicho amesema kimehusisha mawakili wa serikali kutoka mikoa pamoja na halmashauri Tanzania bara.
“Kikao kazi hichi pamoja na mambo mengine kimekuwa na lengo la kuhakikisha miongozo ya utendaji inawafikia mawakili kwa ajili ya utelezaji wa majukumu mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria iliyozinduliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dk Eliezer Feleshi “amesema
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria, George Mandepo, amesema jukumu la la tume hiyo ni sheria zote ili kubaini mapungufu na kupendekeza marekebisho na kutungwa kwa sheria mpya.
“Wizara,Idara zimeanzishwa chini ya sheria fulani hivyo kabla ya kutoa mapendekezo ya kubadilishwa kwa sheria lazima tuangalie kwanza wakati inaanzishwa wakati wa kati na wakati wa sasa ili tuweze kushauri kufanyiwa marekebisho”amesema