Mkurugenzi wa EMICHEM ENTERPRISES Emmanuel Kerato (kulia) akiwa na Mkaguzi Kata wa Kata ya Mabatini Shabani Kashakala (kushoto) katika chumba cha kuhifadhia kemikali zinazotumika kutengenezea bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni .
Mkurugenzi wa Kampuni ya EMICHEM ENTERPRISES Emmanuel Kerato akizungumzia namna wanavyowasaidia vijana,wanawake kupata mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali
Vijana, wanawake wakiwa kwenye mafunzo kwenye Kampuni ya EMICHEM ENTERPRISES
Mkaguzi Kata wa Kata ya Mabatini Shabani Kashakala (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa EMICHEM ENTERPRISES Emmanuel Kerato (kushoto)
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Vijana zaidi ya 60 waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu wamesaidiwa kupata elimu ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamebainishwa na Mkaguzi Kata wa Kata ya Mabani Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Shabani Kashakala wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kampuni ya EMICHEM ENTERPRISES inayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali pamoja na utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali.
Amesema matatizo mengi yanayotokea katika Kata hiyo ikiwemo wizi yanasababishwa na vijana kutokana na kukosa ajira hivyo wakatafuta njia mbadala ya kuwatafutia mafunzo ili waweze kupata ujuzi utakao wasaidia kujipatia kipato.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa EMICHEM ENTERPRISES, Emmanuel Kerato amesema wanatoa mafunzo hayo ili jamii ipate vyanzo vya kujiajili.
Amesema waliwapokea watoto walioletwa na Mkaguzi Kata wa Kata ya Mabatini wakawapa mafunzo ya ujasiriamali yaliyowasaidia kujiajili na kujipatia kipato cha kila siku.
“Tangu kuanzishwa kwa kampuni hii mwaka 2016 hadi sasa tumeishatoa mafunzo kwa watu zaidi ya 1000 na wamefanikiwa kujiajili na wengine wameanzisha viwanda vidogovidogo”
Daniel Nemes ni kijana aliekuwa mtaani ambae alikuwa hana shughuli ya kufanya hali iliyopelekea kujihusiha na matukio ya uhalifu ikiwemo wizi.
“Niliishi mtaani kwa muda mrefu na makazi yangu yalikuwa hayaeleweki kula yangu ilikuwa kwa shida sana, baada ya kukutana na Afande Shabani Kashakala alitusaidia kutuleta kwenye kampuni ya EMICHEM ENTERPRISES kwaajili ya kujifunza mafunzo ya ujasiriamali bila malipo na tumekuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni za maji na miche”,