Mkurugenzi wa taasisi ya tabia nchi na mazingira chuo kikuu cha Agha khan Arusha Dk Emanuel Sule akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha .
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Jamii za pembezoni wakiwemo wakulima na wafugaji kanda ya kaskazini ambazo ziliathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabia nchi,zimeanza kupatiwa elimu kwa vitendo ya namna bora ya kukabiliana na majanga kwa kuwekeza kwenye kilimo mseto.
Taasisi ya masuala ya tabia nchi na mazingira chuo kikuu cha Agakhan Tawi la Arusha wameanza kutekeleza mradi huo kwa lengo mahususi la kuiunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na majanga hayo ambayo yamekuwa yakileta athari kubwa haswa masikini.
Elimu hii inaanzia kwa wanahabari kutoka vyombo mbalilmbali nchini ili waweze kutumia kalamu zao kuhabarisha umma namna bora ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi .
Ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye tawi la Arusha, akizungumza na waandishi wa habari, juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira ili kulinda binadamu,mimea na mifugo, wasipate madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.
Mkurugenzi wa taasisi ya tabia nchi na mazingira chuo kikuu cha Agha khan Arusha Dk Emanuel Sule amesema kuwa , nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ziongeze idadi ya viwanda vinavyozalisha bidhaa zisizoharibu mazingira na kufyonza kaboni kwa Maendeleo Endelevu (SDGs).
Taasisi yetu imejikita zaidi katika kutatua changamoto za mazingira, hasa zinazoathiri jamii zinazoishi ukanda wa kaskazini mwa Tanzania, kutokana na ukame unaoletwa na mabadiliko ya tabia nchi, hivyo tunashauri jamii za maeneo hayo kupanda miti na majani inayohimili ukame, lakini pia wanapata malisho na kuinua uchumi wao.
“Lakini mbali na kupata malisho wanahifadhi mazingira yao kwa sababu inasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo,”amesema.
Amesema katika karne ya sasa, elimu ya kukabiliana na mazingira si ya kukaa darasani pekee, lazima wanafunzi watekeleze kwa vitendo ili kuhakikisha mazingira yanatunzwa.
“Kutokana na Taasisi yetu kujua hili
Tunashirikiana na jamii kwa kupata maarifa asili katika utunzaji wa mazingira ikiwemo mifugo,lakini tunapokea wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali ndani nannje ya nchi kuja kujifunza hapa kwetu kwa vitendo utunzaji wa mazingira,”amesema.
Amesema kwa taasisi hiyo wanayo miti zaidi ya 100, aina tofauti, ikiwemo miti ya mpingo ambayo inathamani kubwa nchini.
Ameongeza kuwa , mabadiliko ya tabia nchi yanaleta athari kubwa kwa wananchi waliopo pembezoni, hivyo kila mmoja anapaswa kulinda mazingira ili kuepukana na athari zake.
Akitoa mfano amesema mwaka huu, nchi za Kenya na Tanzania zilipata athari ya mafuriko ya mvua kubwa ambazo ziliharibu mazingira na kupoteza uhai wa baadhi ya watu,kutokana na watu kukata miti kwa ajili ya shughuli za binadamu.
“Watu wafike mahali lazima wakubali kubadilika kwa kuachana na kilimo kisicho endelevu ikiwemo kutumia nishati mbadala kama vile gesi asilia inayopunguza uchafuzi wa mazingira ikiwemo matumizi ya sola.”amesema.
Mkurugenzi uendeshaji wa vifaa chuo kikuu cha Aghakhan tawi la Arusha,Murad Jivan amesema chuo hicho kimekuja na mradi wa kusaidia jamii kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kuwezesha kuondokana na changamoto za vipindi vya ukame ambavyo husababisha kupoteza mifugo na mazao kukauka au kuzidiwa na mvua.
Baada ya mvua za El nino maeneo mengi nchini yameathirika kutokana na ongezeko la joto na uharibifu wa mazingira hivyo wananchi wengi kujikuta wakipoteza mifugo na maeneo ya malisho ambayo yamepoteza ikolojia ya maeneo hayo.