Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, Julai 15,2024 amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, wakati alipomtembelea ofisini kwake na kujadiliana masuala mbalimbali kuhusiana na hali ya usalama mkoani humo.
IGP Wambura yupo mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi ambapo amekagua gwaride maalum la askari Polisi lililoandaliwa kwa ajili yake na kisha kuzungumza na maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali. Picha na Jeshi la Polisi.