Na Lucas Raphael,Tabora
CHAMA Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa pamba na mazao mchanganyiko (Igembensabo) Igunga Mkoani Tabora kimemshukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwapatia pemmbejeo bure katika kuboresha sekta ya kilimo nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD) yanayofanyika Mkoani hapa, Meneja Mkuu wa Chama hicho Christian Mkude alisema kuwa kuwaishukuru serikali kwa kuwapatia kila kitu bure kwa ajili ya kilimo .
Alisema kuwa maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali ya awamu ya 6 katika sekta hiyo yameleta neema kubwa kwa wanachama wa Igembensabo kwani wameweza kuongeza uzalishaji wa zao lao kuu la pamba kwa kiasi kikubwa sana.
Mkude alifafanua kuwa awali uzalishaji wa zao hilo ulikuwa chini sana akitoa mfano wa msimu wa 2022/2023 ambapo walizalisha kilo mililion 13, msimu wa 2023/2024 kilo mililion 26 na msimu huu wanatarajia kuzalisha kilo mil 30.
‘Haya ni mafanikio makubwa sana, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwa kusimamia vizuri sekta hii, kilimo sasa kina tija kubwa na wakulima wameendelea kunufaika zaidi’, alisema.
Aliongeza kuwa hata bei ya zao hilo na mazao mengine ilikuwa chini sana lakini sasa wana uhakika wa masoko ya mazao yao na bei ni nzuri, alibainisha kuwa msimu huu watauza kilo 1 ya pamba kwa sh 1,400/= tofauti na huko nyuma.
Aidha Mkude alieleza kuwa mafanikio hayo yamechochea wananchi wengi zaidi kulima zao hilo na mazao mengine na vyama vya msingi vya wakulima vimeongezeka kutoka 75 vya mwaka 2022 hadi kufikia 96 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Igembensabo Joseph Mlemeja alisema kuwa katika miaka 3 ya utawala wa Rais Samia uchumi wa wakulima umeinuka zaidi na baadhi yao wameanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo mashine za kukamua mafuta ya alizeti na kusaga na kukoboa mahindi.
Alitaja faida nyingine kuwa ni serikali kuwawezesha kupata trekta za kulimia kwa bei nafuu ambazo zimewapata molari wa kuongeza mashamba na kuwarahisishia upatikanaji pembejeo kwa wakati.
Naye Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani humo Venance Msafiri aliwataka kuendelea kuzingatia maelekezo ya wataalamu ili kufanya kilimo chenye tija kitakachowawezesha kuongeza uzalishaji na kupata mazao bora.