Mkurugenzi mtendaji Archard kato akimuonesha Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo baadhi ya Mvinyo ambao umekwisha kuzalishwa kiwandani hapo.
Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo akipitia kitabu alichokabidhiwa kama zawadi baada ya kuwasili katika kiwanda cha Mvinyo.
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Mvinyo Bw. Archard kato akimuelezea Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo namna ambavyo Mvinyo unazalishwa.
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Mvinyo Bw. Archard kato akimuelezea Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo namna ambavyo Mvinyo unazalishwa.
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Mvinyo Bw. Archard kato akimuonesha Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo baadhi ya miundombinu ya uzalishaji wa Mvinyo kiwandani.
Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kiwandani.
Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo, akizungumza na waandishi wa habari mara ya kutembelea kiwanda cha Mvinyo kinachomilikiwa na mtanzania.
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Mvinyo Bw. Archard kato akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo, kutembelea kiwanda cha Mvinyo kinachomilikiwa na mtanzania huyo.
Na Gideon Gregory, Dodoma.
Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ikiwemo hatua za kikodi walizoziweka kwa mwaka huu ambazo zinalenga kukuza viwanda vya ndani, kusukuma mauzo ya nje kwa bidhaa zinazozalishwa ndani na kuwapa mazingira mazuri wawekezaji ili waendelee kuwekeza nchini.
Prof. Mkumbo ameyasema hayo leo Juni Mosi 2024 Jijini Dodoma wakati alipotembelea kiwanda cha Mvinyo kinachomilikiwa na mtanzania ambapo ameongeza kuwa uwekezaji uliofanyika katika kiwanda hicho ni takribani zaidi ya bilioni 13.
“Tutaendelea kuhamasisha matumizi ya malighafi za ndani ili zisije zikakosa soko la watumiaji pia tutaqngalua na masoko ya nje ya nchi maana masoko yakiwepo zile malighafi za ndani hazitakosa wanunuzi na wawekezaji wengi watakuja kufungua viwanda”, amesema.
Ameongeza kuwa wanachotaka ni kuona mwekezaji anakuwa na sehemu ya kuuza bidhaa zake ndiyo maana wanaendelea kushirikiana nao kwasababu bidhaa wanazozizalisha zinakubalika mbele kama China na hatua inayofuata ni kutafuta soko Ulaya kwamaana bidhaa ikishaingia huko imekubalika dunia nzima.
“Lakini tuna fursa ya soko kubwa la Afrika hili ambalo tumekuwq tukilizungumza maana yake Afrika tuna soko la Bilioni 1.4 kwahiyo mwekezaji huyu tutaendelea kumshawishi ili aweze kupeleka bidhaa zake katika mataifa mengine zaidi ndani ya bara letu hili la Afrika”,ameongeza.
Pia amesema wanatambua kuwa viwanda ndiyo njia sahihi ya kuharakisha maendeleo ya uchumi wa nchi lakini ni muhimu sana kwenye kukuza ajira kwa vijana na dunia kwasasa ina vijana wengi wanaomaliza vyuo mbalimbali kwahiyo hiyo ni njia nzuri ya kusukuma ajira kupitia viwanda.
Mkurugenzi mtendaji Archard kato amesema kwasasa wanauza Mvinyo wao katika masoko yote ya Afrika Mashariki pamoja na China hiyo ikiwa ni namna ya wao kukuza masoko yao ambapo Julai 5,2024 wataenda kufanya ufunguzi rasmi na kuanza uzalishaji pamoja kuingia mkataba wa kuanza kuuza Amerika.
“Lengo letu sisi ni kwenda kwenye masoko ya nje kwasababu tuna utaalamu wa kutosha na Teknolojia za kutosha na rasilimali watu tunayo ya kutosha tukishirikiana nao katika kuhakikisha yote yanaenda vizuri vilevile na ubora wa Mvinyo unaenda vizuri “,amesema.
Aidha ameongeza kuwa upandaji wa dola umekuwa ukiwaathiri pakubwa kutokana na bei wanayouzia Mvinyo ambapo gharama za uuzaji huwa inaongezeka na kiwango cha spiriti kinavyozidi kupanda kinarudisha nyuma kilimo cha zabibu.