Wananchi na wadau wamejitokeza kwa wingi katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika uwanja wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar Es Salaam.
Aidha, katika maonesho hayo Ofisi ya Waziri Mkuu inashiriki pamoja na Taasisi zake na imeendelea kuwaelimisha na kuwafahamisha wananchi na wadau juu ya masuala mbalimbali yanayotekelezwa na ofisi hiyo ikiwemo masuala ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Ustawi wa Watu wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii, Uratibu wa Maafa, Uratibu wa shughuli za Serikali, Ufuatiliaji na tathmini za shughuli za Serikali, Sheria za Uchaguzi, udhibiti wa ukimwi, udhibiti wa dawa za kulevya na fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Taasisi zinazoshiriki katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Fifia kwa Wafanyakazi (WCF), Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC), Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), Baraza la Taifa la Biashara Tanzania(TNBC), Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).
Maonesho hayo ya Sabasaba 2024 yanaongozwa na kauli mbiu isemayo: “Tanzania: Mahali sahihi kwa Biashara na Uwekezaji”