Ametoa maagizo hayo leo katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza,alipotembelea na kukagua banda la MSD katika maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya.
Hapa nchini MSD ina jukumu la kuzalisha,kuhifadhi,kuuza na kusambaza bidhaa za afya zikiwemo dawa tiba za asili ya kulevya.
Awali akiwa katika banda la Shirika lisilo la Kiserikali la ICAP nchini,Mhangama alipata maelezo kutoka kwa vijana (mabalozi) waliokuwa waraibu wa dawa za kulevya ambao baada ya kutibiwa na kupona kwa msaada shirika hilo wameajiriwa kuwa mabalozi wa kutoa elimu ya kupiga vita dawa za kulevya katika jamii.
Waziri huyo wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu ameahidi kulichukua ombi hilo na kulifanyia kazi ingawa awali vijana hao walipewa fursa kusoma katika vyuo vya ufundi stadi (VETA).
Mhagama alikuwa akikagua mabanda ya washiriki wa madhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya yanayofanyika katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza,yatafikia kilele kesho Juni 30, mwaka huu, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.