NA VICTOR MASANGU, PWANI
Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kimejiwekea mipango kabambe ya kuhakikisha kwamba wanapata wagombea wazuri na wenye sifa ambao wanakubalika katika jamii na kuweza kusabisha kuweza kuibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa (CCM) Mkoa wa Pwani Bernad Ghathy wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya (CCM) Mkoa ambapo amesema kuwa lengo kubwa la chama ni kuweka misingi imara ya kuwapata viongozi wazuri ambao watakwenda kuipeperusha vyema bendera ya chama kwa kushinda katika mitaa yote ndani ya Mkoa wa Pwani.
Katibu Ghaty alisema kwamba kikao hicho cha Halmashauri kuu kimeelekeza kwamba katika vikao vyte vya uteuezi vitakavyofanyika katika ngazi ya chama vihakikishe kwamba vinatenda haki bila upendeleo wowote katika kuwapata viongozi ambao watagombea katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa.
“Tumekutana katika kikao cha Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani na hiki kikao ni cha kikatiba kabisa na tumeweza kuzungumzia mambo mbali mbali ya utekelezaji wa ilani pamoja na kupokea taarifa ya serikali ya Mkoa ikionyesha kazi na miradi mbali mbali ambayo imetekeleza katika sekta tofauti, ikiwa sambamba na kujadili hali ya kisiasa katika Mkoa wa Pwani,”alisema Katibu Ghathy.
Aidha Katibu huyo alifafanua kwamba Halmashauri hiyo imempongeza kwa dhati Mwenyekiti wa (CCM) Taifa ambaye pia ndiye Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwatumikia wananchi katika nyanja mbali mballi za miradi ya maendeleo ikiwemo elimu, wananchi kuweza kupata huduma ya maji safi na salama, miundombinu ya barabara sambamba na uboreshawaji wa huduma ya afya.
Kadhalika hakusita kutoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge pamoja na wasaidizi wake kwa kuweza kuhakikisha kwamba wanajitahidi kupambana kuboresha miundombinu ya barabara ili iweze kupitika kwa urahisi hata katika kipindi cha mvua zinaponyesha.
Pia amebainisha kuwa chama cha mapinduzi Mkoa wa Pwani wanajivunia kupata Mwenyekiti wa Taifa ambaye ni msikivu na shupavu kwani ameweza kufanya mambo makubwa mbali mbali ya kukisaidia chama ikiwemo kuchangia katika mradi wa jengo la kitega uchumi ambalo linatarajiwa kuzinduliwa ifikapo Julai 30 mwaka huu na kuanza kutumika.
Katika hatua nyingine amesema kuwa mikakati ambayo wamejiwekea ni kuendeleza sera ya chama ya kuweka mifumo ya kujiimarisha kichumi kuanzia ngazi za chini kwa kushirikiana bega kwa bega na wanachama wote wa chama cha mapinduzi lengo ikiwa ni kuweza kuletaa mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia vitegaa uchumi vilivyopo.