*Amenyanyua kikokotoo, Ndejembi asema huo ni mwanzo tu
Nukuu za Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi-
Bungeni
“Bajeti
Kuu ya Serikali ya Mwaka wa fedha 2024/2025 ambayo tunaenda kuipitisha
inaonyesha ni namna gani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan anaguswa na maisha ya wafanyakazi wa nchi hii. Tangu aingie
madarakani mwaka wake wa kwanza alipandisha madaraja yaliyokwama kwa miaka
mingi, wafanyakazi waliokuwa hawajapandishwa maradaja kwa miaka Tisa (09),
alipandisha zaidi ya watumishi 222,000” – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
“Mheshimiwa
Rais aliguswa sana na madeni kwa watumishi wa Umma, alitoa fedha kwaajili ya
kulipa madeni hayo ya watumishi” – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu –
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
“Julai
2022 kuna mabadiriko ya Kikokotoo yalifanyika, waliokuwa watumishi wa Umma
walitoka kulipwa mkupuo wa Asilimia 50 na kushuka Asilimia 33. Waliokuwa
Asilimia 25 walipanda kwenda Asilimia 33. Ilikuwa ni kilio kwa watumishi ambao
mishahara yao ni ya chini na husubiria mkupuo wa fedha hizi kuanza maisha yao
wanapokuwa wamestaafu” – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
“Wizara
ya Fedha mwaka wa fedha 2024/2025 wameweka Shilingi Bilioni 155 kwaajili ya
kulipa Kikokotoo kunyanyua kutoka Asilimia 33 kwa waliokuwa Asilimia 50 kabla
ya Julai 2022 kwenda Asilimia 40. Waliokuwa Asilimia 25 wamekwenda Asilimia
35” – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
“Wabunge
wengi mmezungumzia suala la kuangalia kiwango kiendelee kunyanyuka kurejea
kilipokuwa Asilimia 50. Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri wameshukuru Asilimia
40 lakini wanaomba iweze kurudi Asilimia 50. Huu ni mwanzo mzuri ndiyo maana
Asilimia 7 imewekwa” – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
“Serikali
itazidi kuangalia ni namna gani itarudi katika Asilimia 50 ya Kikokotoo.
Wanaoenda kulipwa siyo tu wanaokwenda kustaafu kuanzia 01 Julai, 2024. Wanaenda
kulipwa wote hata wale waliostaafu kuanzia Julai 2022” – Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius
Ndejembi
“Watumishi
17,068 toka Julai 2022 wanaenda kulipwa mapunjo yao ya Asilimia 7 waliyostahili
kupata. Waliokuwa wanapata Asilimia 33 kwenda Asilimia 35 watalipwa mapunjo yao
ya Asilimia 2. Tunatarajia kuona wengi wakija kudai mapunjo ya mafao yao”
– Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
Mhe. Deogratius Ndejembi