MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Dk. Eliezer Feleshi,akimsikiliza Mwananchi mara baada ya kuzindua kliniki ya ushauri na elimu ya kisheria kwa umma inayokusudia kusogeza huduma za sheria karibu na wananchi iliyozinduliwa leo Juni 26,2024 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Dk. Eliezer Feleshi,akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kliniki ya ushauri na elimu ya kisheria kwa umma inayokusudia kusogeza huduma za sheria karibu na wananchi iliyozinduliwa leo Juni 26,2024 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Dk. Eliezer Feleshi,akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kliniki ya ushauri na elimu ya kisheria kwa umma inayokusudia kusogeza huduma za sheria karibu na wananchi iliyozinduliwa leo Juni 26,2024 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Dk. Eliezer Feleshi,akisisitiza jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kliniki ya ushauri na elimu ya kisheria kwa umma inayokusudia kusogeza huduma za sheria karibu na wananchi iliyozinduliwa leo Juni 26,2024 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Mary Makondo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kliniki ya ushauri na elimu ya kisheria kwa umma inayokusudia kusogeza huduma za sheria karibu na wananchi iliyozinduliwa leo Juni 26,2024 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
MWANDISHI Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kliniki ya ushauri na elimu ya kisheria kwa umma inayokusudia kusogeza huduma za sheria karibu na wananchi iliyozinduliwa leo Juni 26,2024 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Dk. Eliezer Feleshi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua kliniki ya ushauri na elimu ya kisheria kwa umma inayokusudia kusogeza huduma za sheria karibu na wananchi iliyozinduliwa leo Juni 26,2024 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Dk. Eliezer Feleshi amezindua kliniki ya ushauri na elimu ya kisheria kwa umma inayokusudia kusogeza huduma za sheria karibu na wananchi ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizindua kliniki hiyo leo Juni 26,2024 jijini Dodoma, Jaji Dk. Feleshi amesema pamoja na kufikisha huduma za sheria karibu na wananchi pia itasaidia kufikia malengo ya kupunguza migogoro dhidi ya serikali.
“Kwani wananchi wakisikilizwa na kupata suluhu ya changamoto zao za kisheria dhidi ya serikali hawatakuwa na haja ya kuishitaki serikali katika vyombo mbalimbali vya utatuzi wa migogoro nje ya na ndani ya nchi”amesema Jaji Feleshi
Aidha, ameeleza lengo la kliniki hiyo ni kutekeleza maagizo ya Rais Samia, ambayo amekuwa akiyatoa mara kwa mara kwa viongozi wa serikali kuweka utaratibu wa kusikiliza malalamiko ya wanachi na kuyatatua.
“Ikiwa ni pamoja na kuwaongoza katika taratibu za kupata haki zao pale zinapovunjwa au zinapoonekana kuelekea kuvunjwa na kudumisha utawala bora kwa kuimarisha utawala wa sheria nchini”amesema
Hata hivyo amesema kuwa kusogeza huduma za sheria karibu na wananchi kutasaidia kuongeza utengamano na utulivu katika jamii na kuchochea maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Pia ametoa rai kwa mawakili wote wa serikali kutenga muda na kuwasiliza wananchi katika maeneo yao kupitia kamati za ushauri wa kisheria ngazi za mikoa na wilaya zilizozinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Mary Makondo,amesema kuwa lengo ni kuwasaidia wananchi ambao sisi sote tumepewa dhamana Mhe. Rais ili tuweze kuwahudumia ambapo hilo tunaliona kwa matendo wananchi wanaendelea kutatuliwa kero zao lakini pia kupata ushirikiano kutoka kwa wadau wote.
Naye, Makamu wa rais wa chama cha Mawakili wa serikali Tanzania Bi.Ellen Rwijage,ametoa wito kwa watanzania wote wenye kero zinazohusu masuala ya sheria kujitokeza kupata huduma hiyo bure.
“Mawakili wa serikali wamejipanga kutoa huduma kwa muda wa wiki moja ambao utatumika kusikiliza na kutoa elimu na ushauri wa kisheria.”amesema Rwijage