Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 24.06.2024 imetoa elimu kwa umma juu ya madhara ya matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya katika Kambi Maalum ya Madaktari Bingwa zaidi ya 450 ambao wanatoa huduma za matibabu bure kwa wakazi wa Mkoa wa Arusha katika uwanja wa Sheikh. Amri Abeid Karume jijini Arusha.
Aidha, mgeni rasmi aliyefungua kambi hiyo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda. Katika ufunguzi huo mgeni rasmi alimpigia simu Mhe. Rais wa Nchi, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amepongeza taasisi zote zilizoshiriki katika kambi hiyo na kuahidi Serikali itaangalia nini cha kufanya katika kutia nguvu jitihada zilizofanywa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.