KAIMU Meneja Rasilimali Watu na Utawala kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.Migisha Kahangwa,akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la BRELA wakati wa Maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma 2024 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
AFISA Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.Gabriel Girangay ,akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la BRELA wakati wa Maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma 2024 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) limejikita katika kutoa elimu ya viwango na udhibiti ubora kwa wananchi katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma 2024.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Meneja Rasilimali Watu na Utawala Bw. Migisha Kahangwa ,wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la BRELA katika Maonesho yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Bw.Kahangwa amesema wamekuwa wakitioa elimu kwa wananchi wanaofika katika banda lao kuhusiana na masuala mbalimbali likiwemo kusajili biashara zao hivyo ni muhimu wananchi wapite katika banda hilo ili waweze kusajili .
“BRELA inakuzisha biashara kwa kusajili makampuni , majina ya biashara, alama za huduma na biashara, kutoa leseni za viwanda pamoja na kutoa leseni za biashara daraja `A’ ,”
“Tunawakaribisha wananchi wa mkoa wa Dodoma pamoja na mikoa ya jirani na vitengo vyake waweze kushiriki kwasababu tunatoa huduma moja kwa moja mahali hapa ambapo kila mwananchi anafika kwenye banda letu anapata huduma moja kwa moja na kuondoka pamoja na cheti chake.” amesema Bw. Kahangwa.
Aidha amewataka wananchi kutumia vyema mifumo ya TEHAMA ili waweze kusajili huduma zao ili wafanye biashara zao kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na nchi.
Kwa upande wake Afisa usajili Bw.Gabriel Girangay, amesema kuwa BRELA imekuja katika maonesho ili kuhakikisha wananchi na watumishi wa umma wanaojihusisha na biashara wanasaidiwa kutokana na matatizo ambayo wanakutana nayo katika usajili na shughuli zingine za biashara.
Hata hivyo Bw.Girangay amesema kuwa wamekuwa wakitembelea wafanyabiashara katika maeneo yao ili kutatua changamoto mbali mbali ikiwemo ya elimu juu ya mifumo yao kwani huduma zote zinatolewa kwa njia ya mifumo.
“Kwa sasahivi tunafanya shughuli zetu bila kutumia makaratasi, tunatumia mfumo wa kompyuta kwa upande wa BRELA inaitwa ORS (Online Registration System) ambayo utatumia katika kupata huduma zote za BRELLA ikiwa ni pamoja na kupata taarifa yoyote ya kampuni unayohitaji nchini,”
Giangay ameongeza kuwa, “sheria inamuhitaji kila mfanya biashara ajirasimishe kwasababu ukirasimisha biashara yako unapata faida nyingi ikiwa pamoja na uwezo wa kupata huduma za kibenki, kupata tenda mbali mbali za serikali na sekta binafsi lakini pia kupata ubia kwasababu watu wengine kutoka nje ya nchi wakifika nchini hawaangaiki kusajili kampuni wanachofanya wanawatafuta watu ambao teyari wapo sokoni wanafanya biashara hivyo wanaungana nao.”
Aidha amesisitiza makampuni pamoja na majina ya biashara kuwa na tabia ya kutoa taarifa kila ifikapo mwaka kupitia fomu na 128 ili BRELA iijulishe mtu yoyote anayehitaji taarifa za kampuni kuwa ipo sokoni na inafanya biashara.