Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula, akizungumza leo Juni 18,2024 Jijini Dodoma kwenye Kongamano la kwanza kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lenye dhima ya maendeleo ya sasa katika Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi yaweze kuleta faida endelevu katika viwanda na Jamii.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof.Lughano Kusiluka,akizungumza kwenye Kongamano la kwanza kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lenye dhima ya maendeleo ya sasa katika Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi yaweze kuleta faida endelevu katika viwanda na Jamii.
Rais wa ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati,akizungumza kwenye Kongamano la kwanza kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lenye dhima ya maendeleo ya sasa katika Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi yaweze kuleta faida endelevu katika viwanda na Jamii.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano la kwanza kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lenye dhima ya maendeleo ya sasa katika Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi yaweze kuleta faida endelevu katika viwanda na Jamii.
Na Gideon Gregory, Dodoma.
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amesema kwasasa dunia inapitia mabadiliko makubwa ya Teknolojia kwenye sayansi, ubunifu ambapo kuna mambo mapya mengi yanayotokea lakini Chuo Kikuu Cha Dodoma hakipo nyuma kuendana na mabadiliko hayo.
Dkt. Rwezimula ameyasema hayo leo Juni 18,2024 Jijini Dodoma kwenye Kongamano la kwanza kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lenye dhima ya maendeleo ya sasa katika Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi yaweze kuleta faida endelevu katika viwanda na jamii.
Amesema wanafunzi wa chuo hicho wameonyesha matokeo ya tafiti walizozifanya na jinsi gani wamechangia kwenye jamii ya wasomi huku akiongeza kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma bado kina mchango mkubwa kwa serikali.
“Kwaio nimefika leo kuangalia wanachokifanya, wana maonyesho mazuri, kuna teknolojia wanafanya wamebuni na wanafunzi wanashiriki vizuri na mpango wao mpaka mwaka 2026 kiwe ni chuo namba 1 Tanzania ambacho kitakuwa kimetoa machapisho mengi.” amesema Rwezimula.
Aidha amesema tafiti hizo zinazofanywa na UDOM zimekuwa msaada kwa serikali katika kupata majawabu ambayo yanarahisisha ufanyaji wa kazi.
Kwa upande wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof.Lughano Kusiluka amesema mkutano huo wa kwanza umetayarishwa kwaajili ya kujadili mambo ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu huku ukiarika wanasayansi wabunifu kutoka ndani na nje ya nchi kwenda kujionea na kujifunza juu ya kile wanachokifanya.
“Chuo chetu kina wataalamu katika idara tofauti ikiwemo mambo ya mabadiliko ya tabia nchi, jografia pamoja na kitengo kinachofundisha namna ya kupambana na majanga pamoja na wahandisi wa mambo ya mazingira kwahiyo itakuwa rahisi kwa wageni kuja kwetu kujifunza vitu mbalimbali vinavyohusiana na masuala ya utafiti”,amesema.
Naye Rais wa ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati Saidi Vuai amesema mkutano huo ni zao endelevu la wiki ya CNMS lenye lengo la kuwapa fursa vijana kuweza kuonyesha umahili wao kupitia mafunzo wanayoyapata.
“Tafiti hizi zinatakiwa baada ya kufanywa na kupata matokeo yake ndio ambazo zinaweza zikatoa taarifa kwa wakufunzi namna ya kufundisha lakini pia kutoa matokeo ambayo yanaweza kusaidia kufanya kazinza huduma kwa jamii.” amesema.