NAIBU Makamu Mkuu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Taaluma, Utafiti na Ushauri Prof. Razack Lokina ,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Kongamano la Mtandao wa Ekolojia ya Kisiasa POLLEN2024, linalolenga kushughulikia migogoro ya kijamii na kiikolojia katika kuchunguza njia za kufikia mustakabali wenye haki na utofauti zaidi.
NAIBU Makamu Mkuu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Taaluma, Utafiti na Ushauri Prof. Razack Lokina ,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kufungua Kongamano la Mtandao wa Ekolojia ya Kisiasa POLLEN2024, linalolenga kushughulikia migogoro ya kijamii na kiikolojia katika kuchunguza njia za kufikia mustakabali wenye haki na utofauti zaidi.
MHADHIRI Mkuu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Idara ya Jiografia na Stadi za Mazingira Dkt. Mathew Mbele,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Kongamano la Mtandao wa Ekolojia ya Kisiasa POLLEN2024, linalolenga kushughulikia migogoro ya kijamii na kiikolojia katika kuchunguza njia za kufikia mustakabali wenye haki na utofauti zaidi.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia Kongamano la Mtandao wa Ekolojia ya Kisiasa POLLEN2024, linalolenga kushughulikia migogoro ya kijamii na kiikolojia katika kuchunguza njia za kufikia mustakabali wenye haki na utofauti zaidi.
Na Gideon Gregory, Dodoma.
NAIBU Makamu Mkuu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Taaluma, Utafiti na Ushauri Prof. Razack Lokina ameongoza kongamano la Mtandao wa Ekolojia ya Kisiasa POLLEN2024, linalolenga kushughulikia migogoro ya kijamii na kiikolojia katika kuchunguza njia za kufikia mustakabali wenye haki na utofauti zaidi.
Kongamano hilo linafanyika kuanzia leo Juni 10-12,2024 katika maeneo matatu ambayo ni Dodoma (Tanzania), Lima (Peru), na Lund (Sweeden) likiwa na kaulimbiu “Kuelekea Mustakabali wa Utofauti na Haki,” ambapo inalenga kukuza mazungumzo na kubadilishana mawazo kati ya tamaduni tofauti za ekolojia ya kisiasa, maeneo tofauti kijiografia, na kati ya wasomi na jamii kwa ujumla.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa kongamano hilo Prof. Lokina amesema kongamano hilo pia linaangalia namna wananchi wanaweza kutunza ikolojia kwani ndiyo mfumo mzima wa kimazingira katika kuweka mahusino sawa kati ya viumbe na Wanyama katika katika mazingira.
“Kongamano hili linatusaidia katika kujifunza vitu mbalimbali kutoka kwa wenzetu na kutokana na utofauti uliopo wa hali ya hewa kati ya Afrika na Mabara mengine kuliko ile kuwa na utafiti wa upande mmoja ambao mwisho wa siku matokeo yanakuwa hayana tija kluliko ile tukishirikiana na wenzetu,” amesema.
Kwa upande wake Mhadhiri wa Mkuu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Idara ya Jiografia na Stadi za Mazingira Dkt. Mathew Mbele amesema msingi wa kufanya kongamano hilo Tanzania ni kutokana na tafiti nyingi za masuala ya uhifadhi wa wamazingira zinafanyika hasa katika mabara hayo matatu huku mawasilisho yake yakiwa yanafanyika katika bara la ulaya ila kuanzia sasa wanataka zianze kuwasilishwa katika mabara zinapofanyikia.
“Mpangilio huu wa kuwa nan chi Tatu unatokana na namna ya mpangilio wa tafiti za kiakademia mara nyingi imekuwa ikifanyika katika nchi za ulaya na katika nchi hizo za ulaya kunakuwa na changamoto moja inayopelekea washiriki kushindwa kushiriki kutokana na kukosa fedha ndiyo maana mwaka huu tukafanya hivi”,amesema.