Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Osiligilai Maasai Lodge Ltd,William Mollel akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha kwenye maonyesho ya Karibu -Kilifair yanayoendelea mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Osiligilai Maasai Lodge Ltd,William Mollel akizungumza na na mmoja wa watalii aliyefika kwenye banda lake kupata maelezo kuhusu kampuni hiyo kwenye maonyesho ya Karibu -Kilifair yanayoendelea mkoani Arusha.
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha.Kampuni inayojishughulisha na utalii ya Osiligilai Maasai Lodge Ltd,iliyopo Sanya juu mkoani Kilimanjaro imeanzisha taasisi maalumu.kwa ajili ya kuwasaidia wasichana wa jamii ya kimasai wanaotoka kwenye mazingira magumu kuweza kupata elimu bure .
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha katika maonyesho ya utalii ya Karibu -Kilifair, Mkurugenzi wa kampuni hiyo,William Mollel amesema kuwa ,amekuwa na ndoto ya kuanzisha shirika hilo kwa lengo la kuwasaidia watoto wa jamii ya kifugaji kuweza kupata elimu kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kuozeshwa wakiwa wadogo.
Amesema kuwa,Taasisi hiyo ijulikanayo kwa jina la Maa Eagles Foundation imekuwa mkombozi mkubwa sana kwa watoto hao ambapo hadi sasa hivi ina jumla ya wasichana wa jamii hiyo 70 ambao wanahudumiwa na taasisi hiyo.
“Tumeamua kunzisha taasisi hii kwa lengo la kuwasaidia watoto waweze kupata haki zao za msingi na kuweza kuondokana na mila na desturi zilizokuwepo za kuwaozesha wasichana hao wakiwa umri mdogo jambo ambalo wanakosa haki zao za msingi”amesema .
Amefafanua zaidi kuwa,kabla ya kuanzisha taasisi hiyo walikuwa wakisaidia wasichana wengi wa jamii hiyo ambapo idadi kubwa walishahitimu masomo yao na wengine wapo chuo kikuu .
“Kupitia utalii tunaofanya wageni wanapofika katika lodge yetu wanakutana na maswala mbalimbali ya kiutamaduni wa jamii ya kimasai na kile kinachopatikana tunaendelea kusaidia jamii ili nao wanufaike na uwepo wa kampuni hiyo.”amesema .
Ameongeza kuwa ,eneo hilo wanapokuja watalii kupumzika sio sehemu ya kulala tu bali ni sehemu ya maajabu ambayo wanafika na kuweza kujifunza mila za jamii ya kimasai ikiwemo kufundishwa namna ya kurusha mishale na namna ambayo wamasai wanavyoweza kuua Simba kwa kutumia mishale.
Ameongeza kuwa, katika eneo hilo ndilo sehemu pekee mtalii ataweza kufika na kujionea maajabu makubwa ya mila.na desturi zinazofanywa na jamii ya kifugaji na kuweza kujifunza maswala mbalimbali ya mila na desturi hizo.
“Lengo kubwa la kampuni yetu ya utalii ya Maasai ni kutangaza utalii ndani na nje ya nchi ikiwa ni njia mojawapo ya kumuunga mkono Rais wetu katika kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii kwani Rais Samia ni mfano wa kuigwa kwa namna ambavyo anapambana kukuza utalii na kufanya idadi kubwa ya watalii kuendelea kuongezeka siku hadi siku.”amesema Mollel.
Aidha amewataka watalii mbalimbali kufika katika eneo hilo ili kuweza kujifunza mila na desturi za jamii ya kimasai kwani lengo kubwa ni kuendelea kuenzi na kudumisha mila zetu.