Waziri wa Maliasili na utalii, Angellah Kairuki akizungumza katika.uzinduzi huo mkoani Arusha
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Waziri wa Maliasili na utalii, Angellah Kairuki amesema dhamira ya serikali ni kuendelea kuutangaza utalii wa Tanzania duniani kote ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja kutalii nchini.
Ameyasema hayo mkoani Arusha wakati akizindua maonesho ya Karibu-Kili Fair kwenye Viwanja vya Magereza Mjini Arusha.
Amesema serikali pia inatambua mchango wa sekta binafsi katika jitihada za kukuza na kuutangaza utalii wa Tanzania.
Aidha Kairuki amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuutangaza utalii kupitia Makala ya The Royal Tour na Amaizing Tanzania suala ambalo limeongeza idadi ya watalii wanaofika kutalii nchini Tanzania.
Waziri Kairuki ameahidi kuendelea kushirikiana na wadau wa utalii wakiwemo mawakala wa usafiri ili kuhakikisha wanawezeshwa na wanakuwa sehemu ya mabalozi wa utalii watakaokuwa na jukumu la kuutangaza utalii wa Tanzania.
“Kipekee naipongeza Kampuni ya Kili Fair Promotion Ltd kwa kuandaa maonesho ya Karibu Kili Fair 2024, onesho ambalo limekuwa likiongeza idadi ya watalii wanaofika nchini Tanzania na kuifahamisha dunia kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania”amesema Kairuki.
Aiidha wadau mbalimbali wa utalii wakishiriki ni kutoka Tanzania, Ghana,Burundi, Cameroon na Afrika Kusini huku makampuni zaidi ya 700 kutoka nchi zaidi ya 40 wakishiriki”amesema.
“Maonyesho hayo yatakayodumu kwa siku tatu mfululizo yanatoa fursa ya kiuchumi kwenye sekta ya kilimo, Usafiri, utalii pamoja na kubadilishana uzoefu kutokana na wingi wa wageni na wadau wa utalii wanaotarajiwa kuhudhuria maonesho hayo makubwa kwa Afrika Mashariki” amesema Shoo.
Kwa upande wake Waziri wa Utalii na Malikale Zanzibar, Mhe. Mudrik Soraga amesema kuwa kuna haja ya kuendelezana kuwa na mkakati mzuri wam awasiliano ambao utakuwa unaweza kutoa taarifa kwa mgeni na kuweza kuona kwamba anapokuja Zanzibar anaweza kuja Arusha ama anapokuja Arusha anaweza kwenda Zanzibar.
Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaahidi itaendelea kushiriki katika matukio makubwa ya kutangaza utalii kama hayo kwa sababu inaleta hamasa kwa sekta ya utalii kwa pamoja.