Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Na Gideon Gregory, Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameziagiza Halmashauri zote, kusimamia ipasavyo utekelezaji wa sheria ndogo za kulinda mazingira na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya wanaokwenda kinyume na sheria huizo.
Dkt. Mpngo ameyasema hayo leo Juni 5,2024 Jijini Dodoma kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ilichokwenda sambamba na uzinduzi wa Sera ya Uchumi wa Buluu kikiwa na kauli mbiu inayosema “Urejeshwaji wa Ardhi, Ustahimilivu wa hali ya jangwa na ukame” na kuongeza kuwa kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake katika kuhakikisha hakuna mwananchi anayetupa taka hovyo na kuchafua mazingira.
“Kifungu cha 89 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288, kinazipa Halmashauri mamlaka ya kutunga sheria ndogo za Utunzaji wa Mazingira na Udhibiti wa Taka.icha ya kuwepo kwa Sheria ndogo zilizotungwa kukabiliana na changamoto hiyo na kuhakikisha miji yetu inakuwa safi, bado taka za aina mbalimbali zinazagaa hovyo mitaani”,amesema.
Pia amesisitiza umuhimu wa kubadili kilimo ili kiwe endelevu na cha kisasa zaidi, kinachozingatia matumizi ya mboji na marejea, matumizi ya matandazo ya majani ili kuhifadhi unyevu, matumizi ya teknolojia za kijani pamoja na kudhibiti uchomaji hovyo wa misitu na vichaka.
Ameongeza kuwa ili kufanikiwa kupunguza na hatimaye kukomesha kabisa uharibifu wa mazingira, lazima watafsiri maneno yao kuwa vitendo katika usimamizi wa mazingira (walk the talk) na kuimarisha ushirikiano wa dhati kati ya Serikali, AZISE, Sekta Binafsi na wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Waziri Mkuu,Mhe. Kassim Majaliwa,amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu inakumbusha umuhimu wa kutunza mazingira kwa kizazi cha Sasa na baadae.
“Kasi ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira iende sambamba na kuwashirikisha wananchi wote na kusisitiza suala la utunzaji wa mazingira katika maeneo yetu ili kuendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi tunayoyashuhudia kwasasa”,amesema.
Tunapoadhimisha siku ya mazingira Duniani nitoe wito kwa watanzania kuendelea kutunza mazingira kwani suala hili ni ajenda muhimu ambayo sio tu viongozi wanapaswa kuliongelea bali ni wajibu wa kila mmoja kupitia nafasi yake aliyonayo kwenye jamii.
Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo,amesema kuwa Sera Mpya ya uchumi wa buluu itakayoenda kusaidia wizara za kisekta kuweza kutekeleza majukumu yao.
Akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Naibu Katibu mkuu John Mongella amesema kuwa serikali imefanya vizuri kutekeleza ilani ya chama, kupitia ofisi ya makamu wa Rais wanaona kazi kubwa inafanyika pamoja na Bunge kuhusu suala zima la utanzaji wa mazingira na kuhakikisha kila mtanzania anendelea kushiriki vyema katika zoezi hilo.
“Tunatumai nchi itaendelea kuneemeka zaidi na utunzaji wa mazingira katika kukabiliana na mabadiriko ya tabia ya nchi”, amesema.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mazingira na Usimamizi wa Kijamii wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Bi. Zafarani Madayi kuhusu miradi mbalimbali ya upandaji miti pembezoni mwa Barabara wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt. Ladislaus Chang’a kuhusu maboresho yaliyofanywa katika Taasisi hiyo yanayowezesha utabiri sahihi wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishuhudia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kutokana na taka za plastiki alipotembelea banda la Umoja wa Wazalishaji Vinywaji (PETPro) wakati akikagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya kukagua mabanda ya maonesho katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akitoa maelezo kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma leo tarehe 05 Juni 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Sera ya Uchumi wa Buluu ya Mwaka 2024 mara baada ya kuizindua wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Zahor Kassim El- Kharousy Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya Mwaka 2024 mara baada ya kuizindua wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Kiongozi wa Machifu kutoka Mkoani Mbeya Chifu Rocket Masoko Mwanshinga Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya Mwaka 2024 mara baada ya kuizindua wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa zawadi ya Tuzo ya Mazingira kwaajili ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wake katika uhifadhi mazingira na uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kitaifa na kimataifa. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko mfano wa hundi ya shilingi Bilioni 14.2 iliyotokana na biashara ya kaboni wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.