Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametembelea na kukagua mabanda mbalimbali ya maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Juni 04, 2024.
Amejionea maandalizi ya kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika Juni 05, 2024 ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Akizungumza na wadau alipotembelea mabanda ya maonesho, Dkt. Jafo ametoa wito kwa wadau wa nishati safi ikiwemo ya gesi kupanua wigo wa utoaji wa huduma hiyo ili kila moja amudu kutumia.
Akizungumza na wadau wa Kampuni ya Oryx na UpEnergy amesema Serikali inatambua juhudi zao katika kutia huduma ya nishati safi ya kupikia.
Dkt. Jafo amewaomba waendeleze jitihada hizo na kwa bei ambayo wananchi watamudu ili waachane na matumizi ya kuni na mkaa katika kupikia kwani yanasababisha uharibifu wa mazingira kwa kukata miti.
Akizungumza alipotembelea banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) amepongeza kwa hatua ya kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kuachana na matumizi ya kuni na mkaa kwa kupikia na kuanza kutumia nishati safi.
Amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais iliweka katazo la matumizi ya kuni na mkaa kwa taasisi zinazolisha watu Zaidi ya mia moja kuanzia Januari 2024 na tayari taasisi zimetekeleza maelekezo hayo.
Dkt. Jafo ametumia fursa hiyo kutembelea mabanda mbalimbali yakiwemo ya Mamlaka ya Maji Mijini na Vijijini (RUWASA), Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Magereza, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Chama cha Mazingira na Ufugaji wenye Tija (CHAMAUTA).
Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani kinatarajiwa kufanyika Juni 05, 2024 katika Kituo cha Mikitano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Hivyo kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani kwa mwaka 2024 inasema “Urejeshwaji wa ardhi, Ustahimilivu wa Hali ya Jangwa na Ukame