NJOMBE,
Mkuu wa wilaya ya Njombe KIssa Gwakisa Kasongwa amemtaka Wakili wa Serikali mkuu Candid Nasau kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kusaidia Kutoa mwelekeo wa kisheria na ushauri kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya viongozi wa Chama Cha msingi cha ushirika cha Lupembe Division Saccos kilichopo wilayani Njombe baada ya kuonekana hakina fedha licha ya wanachama kuweka amana zao zaidi ya milion mia tano katika chama hicho.
Mh Kissa ametoa agizo hilo alipokutana na viongozi wa Lupembe SACCOS akiwa na wataalamu wa masuala ya sheria walioweka kambi ya siku 10 mkoani Njombe kutoa usaidizi wa sheria kwa waananchi kupitia kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ambapo amesema imekuwa ngumu sana kwake kutulia ofisini na kisha kulazimika kuwakabidhi wataalamu wa sheria jambo hilo kwasababu wananchi ambao ni wakulima wameweka fedha zao zaidi ya mil. 500 lakini pindi wanapohitaji kuzichukua inaonekana saccos haina hela.
“Nawaomba nyie wanasheria mtusaidie kwenye jambo hili haiwezekani watu wameweka mil 500 lakini wanapohitaji hata elfu moja hakuna ,siwezi kuwa na kicheko na siwezi kuwa na sura ya kirafiki “alisema DC Njombe Kisa Kasongwa.
Ili Kumaliza tatizo hilo Mkuu hiyo wa wilaya amewataka wanasheria kuwahoji kwa karibu viongozi wwa chama hicho na kisha kurikiana kwa karibu na afisa ushirika wilaya ili kupata suluhisho litakalo saidia viongozi kurudisha fedha za watu walizoweka amana.
Wakitoa ufafanuzi kuhusu sababu ya kufilisika kwa saccos hiyo baadhi ya viongozi akiwemo Haji Lugenge ambae ni muhasibu na Neema Edwin mwenyekiti wamesema ni kutokana na kusuasua kwa biashara ya chai ambayo ilisababisha muwekezaji kushindwa kulipa wakulima fedha kwa wakati jambo ambalo lilisababisha kuanza kujiendesha kwa hasara kwasababu watu hawakuendelea kuweka fedha na badala wake walikuwa wakitoa tu .
Wamesema kutokana na wanachama kushindwa kuweka fedha wakalazimika kuanza kukopesha dhamana za watu hadi chama kikafika kwenye hali hiyo ambapo hadi sasa kimebaki na shilingi milioni tatu tu.
Kwa upande wake afisa Ushirika wilaya ya Njombe Fred David amesema njia pekee ya kuirejeshea uwezo na mtaji saccos hiyo ni kumtumia dalali kushika mali za wanaodaiwa na kisha kupiga mnada ili fedha itakayopatikana irudishwe kwenye mfuko wa chama.
Baada ya kuwasikiliza viongozi wa chama ,maoni ya kamati ya ulinzi na usalama wilaya pamoja na maagizo ya mkuu wa wilaya Candid Nasua Wakili wa serikali mkuu akashauri mambo kadhaa ikiwemo kuomba mkopo na kuweka rehani jengo la ofisi lenye thamani ya mil 59,kuomba mkopo na kuweka rehani salio lao na kuanza kukoposha ili kutengeneza faida huku jambo lingine likiwa ni kuingia mkataba na dalali kufuatilia madeni ya mil 350 ili kulipa wana chama wanaodai fedha zao.
Ushauri mwingine uliotolewa na wataalamu hao wa masuala ya kisheria ni Kufanya ukaguzi maalumu ili kubaini uhalisia wa upotevu wa fedha huku wakitaka zoezi hilo kufanyika ndani ya wiki moja likiongozwa na mrajisi.