NAIBU Gavana wa Tanzania Dkt .Yamungu Kayandabila akifungua semina hiyo ya bodi ya NBAA mkoani Arusha
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA.Pius Maneno akizungumza na waandishi wa habari katika semina hiyo.
Mhasibu wa Mradi wa Julius Nyerere (TANESCO) Sarah Mlay akizungumzia kuhusiana na semina hiyo
Washiriki mbalimbali wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zinazotolewa mkoani Arusha .
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .NAIBU Gavana wa Tanzania Dkt .Yamungu Kayandabila amefungua rasmi semina ya Bodi ya wahasibu na wakaguzi Tanzania (NBAA) ambayo imeandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Aidha Dkt .Kayandabila akizungumza katika semina hiyo amesema kuwa semina hiyo ni muhimu sana kwao kwani wanajadili mada yenye umuhimu mkubwa kwa sekta yetu ya fedha na mustakabali wa taifa letu.
Amesema kuwa ,”Mabadiliko ya Kidijitali kwa Huduma Endelevu za Kifedha na Utoaji Taarifa”katika mazingira yanayoendelea kwa kasi ya karne ya 21, mabadiliko ya kidijitali si chaguo tu bali ni lazima.
Ameongeza kuwa ,sekta ya fedha, inasimama katika mstari wa mbele katika mabadiliko haya, kuunganisha
nguvu ya teknolojia ya kidijitali ili kuimarisha utoaji wa huduma, kuboresha
ufanisi, na kuhakikisha uendelevu.
Amefafanua kuwa,semina hiyo inalenga kuzama ndani vipengele hivi muhimu na kuchunguza jinsi wanavyoweza kutumia dijitali kwa pamoja ubunifu wa mfumo ikolojia thabiti na unaostahimili hali ya kifedha.
“Mabadiliko ya kidijitali katika huduma za kifedha ni safari yenye mambo mengi
inajumuisha vipengele mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupitishwa kwa benki ya kidijitali majukwaa, ujumuishaji wa uchanganuzi wa hali ya juu, na utumiaji wa teknolojia.”amesema .
Amesema kuwa,Ubunifu huu unabadilisha njia ya kifedha taasisi zinafanya kazi, na kuziwezesha kutoa zaidi kupatikana huduma za uwazi na ufanisi kwa wateja wao.
Hata hivyo amesema kuwa, faida za mabadiliko ya kidijitali ni uwezo wake Moja ya muhimu zaidi huduma za kifedha ambazo hazijafikiwa kuendesha ushirikishwaji wa kifedha Kwa kupanua benki ya simu na nyingine za kidijitali na jumuiya za mbali kupitia
njia tunaweza kuhakikisha kwamba watu binafsi zaidi na biashara kuwa na upatikanaji wa huduma za kifedha na bidhaa wanazohitaji kustawi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA.Pius Maneno amesema kuwa, semina hiyo inatolewa
Wahasibu, Wakaguzi wa Hesabu, Mabenka, wanafunzi na watu wengine wanaojighulisha na taaluma hiyo.
CPA. Maneno amesema semina hiyo ni muhimu kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayowataka watumishi katika Idara mbalimbali za Fedha kuendana nayo.
“kwa zaidi ya miaka 15 mkutano kama huu umekuwa ukifanyika na kuwapa nafasi watendaji idara za fedha nchini kujadili mambo muhimu yanayohusiana na fedha na mabadilko kidigitali katika utoaji huduma.”amesema .
Aidha mada mbalimbali zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na Mabadiliko ya kidigitali katika utoaji huduma za kifedha za kifedha na taarifa za fedha, Wakaguzi wa ndani na miongozo iliyopo kidigitali, majukumu ya wakaguzi, wahasibu na mabenka katika matumizi ya fedha haramu, Maendeleo endelevu kidigitali katika masoko ya hisa na kutambua fedha zilizotakatishwa.
Kwa upande wake Mhasibu wa Mradi wa Julius Nyerere (TANESCO) Sarah Mlay ambaye ni mmoja wa washiriki wa semina hiyo amesema semina hii ni muhimu na itawaongezea ujuzi, na ufanisi juu ya mabadiliko na maendeleo ya kidigitali na imekuja muda muafaka kwani itaweza kuboresha utendaji kazi wao wa kila.siku.
Mlay amefafanua kuwa ,moja ya mada zinazotolewa ni elimu namna ya kupambana na fedha haramu iliyotakatishwa, hii ni namna gani tunatakiwa kwenda kama dunia inavyotaka katika maendeleo na ukuaji wa teknolojia” amesema Mlay.