Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa Mkutano wa kwanza wa Sayansi za afya uliondaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kuhakikisha afya bora kwa wote hafla iliyofanyika wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Na Gideon Gregory, Chamwino.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewahimiza wananchi kuweka mkakati wa kufanya mazoezi kwa lengo la kuweka sawa miili yao ili kukabiliana na magonjwa ambayo yamekuwa yakiwa kumba mara kwa mara.
Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo leo Wilayani Chamwino kwenye mkutano wa kwanza wa sayansi za afya uliondaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kuhakikisha afya bora kwa wote.
“Lakinj wapo ambao hata hayo mazoezi ya kutembea hawafanyi kwahiyo niendelee kutoa shime suala la mazoezi liwekewe mkakati nakumbuka tuliwahi kukakaa kwenye kikao tukaazimia maafisa ustawi wa Jamii kwenye kila kata watafute eneo wawawekee wazee walau mara moja kwa wiki kuwakutanisha ili wafanye mazoezi yanayoendana na umri wao”,amesema.
Pia amewaomba wananchi kuendelea kuhamasishana ili wajitokeze kwenda kupima Afya zao na kujua mapema juu ya kile kinachowatatiza kabla ya ugonjwa haujawa mkubwa na kuweza kutibiwa mapema.
Aidha, ameongeza kuwa elimu ya afya inapaswa kuendelea kutiliwa makazo kwani ni nyenzo muhimu ya katika kupambana na magonjwa yasiyo ambukiza na kuimarisha ustadi wa kimaisha huku akiongeza kuwa wananchi hawana budi kuzingatia ulaji ulio bora.
“Elimu ya Afya ni nyenzo muhimu katika mapambano dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza, elimu ya mabadilikoa ya mtindo wa maisha ususani ulaji unaofaa, umuhimu wa mazoezi na aina zake, madhara ya utumiaji wa tumbaku na mazao yake, unywaji hatarishi wa pombe na njia zake na kuepukana na msongo wa mawazo unaosababisha magonjwa yasiyo ambukiza yatafundishwa na wataalam waliobibea katika maswala haya”, ameongeza.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Albino Tenge amesema kuwa moja kati ya lengo kuu la mkutano huo ni kutimiza lengo la tatu la maendeleo endelevu la umoja wa mataifa linalolenga maisha yenye afya bora na ustawi kwa watu wote.
“Tuna ushahidi wa kutosha kwamba magonjwa yasiyo ambukizwa kama vile moyo, kisukari, shinikizo la damu la juu na magonjwa mengine yameongezeka duniani kote na athari zake wote tunaziona na zimekuwa kubwa zaidi hasa katika nchi za kipato cha chini na kati”,amesema.
Ameongeza kuwa katika zoezi hilo wanategemea kuwafikia watanzania 1000 mpaka 1793
lengo likiwa ni kuongeza ufahamu kwa wananchi kuhusu magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kushirikiana na Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma kimendaa siku mbili za Uchunguzi wa kibingwa Bure unaofanyika katika Hospitali ya Uhuru iliyopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akikagua mabanda mbalimbali yaliyoandaliwa kwenye mkutano wa kwanza wa sayansi za afya uliondaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kuhakikisha afya bora kwa wote hafla iliyofanyika wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa Mkutano wa kwanza wa Sayansi za afya uliondaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kuhakikisha afya bora kwa wote hafla iliyofanyika wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Janeth Mayanja,akizungumza wakati wa Mkutano wa kwanza wa Sayansi za afya uliondaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kuhakikisha afya bora kwa wote.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Albino Tenge,kwenye Mkutano wa kwanza wa Sayansi za afya uliondaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kuhakikisha afya bora kwa wote hafla iliyofanyika wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Muonekano wa Jengo la Hospitali ya Uhuru iliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa kwanza wa Sayansi za afya uliondaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kuhakikisha afya bora kwa wote hafla iliyofanyika wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.