Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa semina kwa wabunge kuhusu utendaji wa Shirika la Viwango Taanzania (TBS) na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) iliyofunguliwa na Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu (kulia) kwenye Ukumbi wa Msekwa bungeni Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WABUNGE wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepewa elimu juu ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi mbili zilizochini ya Wizara ya Viwanda na Bishara ambazo ni Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).
Akifungua semina hiyo Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Zungu,amesema Bunge linatambua namna TBS inavyopambana kuhakikisha ubora wa bidhaa unazingatiwa na BRELA imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
“Sisi kama wabunge tunazipongeza taasisi hizi mbili TBS na BRELA kwa kutupatia semina hii ambayo imetupa mwanga jinsi mnavyofanya kazi tunawapongeza kwa ubunifu wenu kwa kutoa huduma bora kwa wananchi endeleeni kutoa elimu ili kila mtu ajue majukumu yenu”amesema Mhe.Zungu
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Bunge wa Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Dk Medard Kalemani aliipongeza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuzifanyia mageuzi makuubwa taasisi za TBS na BRELA ambazo zilikuwa na changamoto kubwa ya kiutendaji.
Aidha akijibu hoja za wabunge, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji amewatoa hofu wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo kuhusu Soko la Afrika Mashariki lililopo katika jengo la China Plaza, Ubungo jijini, Dar es Salaam kuwa halitaua biashara zao.
Dk.Kijaji amesema tayari serikali imekaa vikao na wafanyabiashara hao kwa zaidi ya mara tatu kujadiliana kuhusiana na jambo hilo.
“Timu ya Serikali ipo kazini inafanya kazi yake na katika jengo la Ubongo Plaza yanajengwa maduka 2002,wakati Kariakoo kuna maduka 40,000.”amesema Dk.Kijaji
Akijibu hoja za wabunge zilizoibuka kwenye semina hiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Leseni wa BRELA ,Andrew Mkapa amesema kuwa kuna haja ya kutoa elimu kwa watanzania ili wajue haki zao wakati wanaingia ubia na wawekezaji wa nje ya nchi wakati wa kusajili kampuni na kwamba ni vigumu kujua kama mtanzania atadhulumiwa pia wanapofika kusajili kampuni na wageni hao.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk. Athuman Ngenya amesema shirika hilo litaendelea kuboresha miundombinu na kuweka mazingira rafiki ya utoaji wa huduma kwa wakati ili kuchochea ufanyaji wa biashara na kuinua uchumi wa viwanda.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Godfrey Nyaisa alisema katika kipindi cha miaka saba kupitia mfumo wa usajili kieletroniki (ORS), kuna ongezeko la makampuni yaliyosajiliwa kutoka 119,000 hadi kufikia 205,000 Mei mwaka huu
Semina hiyo ina lengo la kueleza utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara katika mwaka wa fedha 2019/20 hadi 2023/24.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa semina kwa wabunge kuhusu utendaji wa Shirika la Viwango Taanzania (TBS) na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) iliyofunguliwa na Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu (kulia) kwenye Ukumbi wa Msekwa bungeni Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu akifungua semina hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Kilimo, Dkt Medard Kalemani akiongoza semina hiyo.
Mbunge wa Mchinga, Mama Salma Kikwete akiwa na Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango TGanzania (TBS), Dkt Yusuph Ngenya akielezea kuhusu utendaji wa shirika hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Biashara na Leseni, Godfrey Nyaisa akitelezea mbele ya wabunge kuhusu utendaji wa wakala hiyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang’ata (kushoto) akiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Massaburi.
Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka na Agnes Hokololo
Wabunge wakiwa kwenye semina hiyo.