Upishi wa kutumia kuni na mkaa kwa wakazi wa kijiji cha Msomera, wilayani Handeni Mkoa wa Tanga unakuwa ni historia mara baada ya wakazi hao kupatiwa majiko banifu na mitungi ya gesi ya kupikia.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi majiko hayo katika Kijiji hicho jana Mei 17, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema kuwa ugawaji wa mitungi hiyo ya gesi na majiko banifu ni miongoni mwa mikakati endelevu ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha ifikapo 2034, asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.
Kapinga pia amewataka wananchi wa kijiji hicho wanaibeba ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo ili kulinda mazingira huku akisisitiza ajenda hiyo inafanikiwa kutokana na ushirikiano mubwa wa Rais Samia.