Shamba la mtama unazalishwa na wakala wa mbegu bora za kilimo ASA katika shamba la kilimi wilayani nzega mkoani Tabora
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt. Sophia Kashenge akiongea na waandishi wa habari katika shamba la mahindi mbegu T105yanayozalishwa katika shamba hilo wilayani nzega
Na Lucas Raphael,Tabora
Wakala wa Mbegu za kilimo ASA umevuka Malengo Uzalishaji wa Mbegu za kilimo katika Mashamba yake kutoka Tani 6,000 zilizokuwa zikitarajiwa hadi kufikia Tani 7,600 Kwa mwaka wa kilimo 2022/2023.
Kauli hiyo iliotolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt. Sophia Kashenge katika Mafunzo kwa maafisa Kilimo na Waendesha Mitambo wa mashamba yote ya wakala wa mbegu yaliyofanyika katika Shamba la Wakala wa Mbegu Kilimi Nzega Mkoani Tabora.
Alisema kwamba Wakala wa Mbegu pamoja na makampuni yanayozalisha Mbegu ndani ya Mashamba ya Wakala kwa pamoja wamevuka Malengo ya Uzalishaji yaliyowekwa kwenye mradi wa Programu ya TFSRP (P4R), Tathmini ya mradi huo imeonyesha wakala kuvuka lengo la uzalishaji wa mbegu kwa asilimia ya zaidi ya 128%.
Alisema kupitia Mradi wa TFSRP (P4R) Wakala ulipangiwa kufikia Malengo ya Uzalishaji wa Tani 6,000 pamoja na makampuni yanayozalisha Mbegu katika Mashamba ya Wakala.
Aidha Wakala pamoja na makampuni hayo umeweza kuzalisha zaidi ya Tani 7,600 za mbegu za Mazao mbalimbali hali hiyo imepelekea kuvuka Malengo ya Uzalishaji kupitia Mradi huo hali iliyopelekea kupata ziada ya fedha za maendeleo ikiwa moja ya ahadi ya programu baada ya kufikia na kuvuka malengo (Program for Result)
Alisema Malengo ya Mradi huo Kwa mwaka wa kilimo 2023/2024 nikufikia Tani 9,000 ikiwa ni ASA pamoja na makampuni yanayozalisha Mbegu ndani ya Mashamba ya Wakala.
Dkt. Sophia alisema Wakala Kwa msimu huu unatarajia kuzalisha Mbegu zaidi ya Tani 8,500 kwa Mazao yote, hivyo ikijumuishwa na mbegu zitakazozalishwa na sekta binafsi katika Mashamba ya ASA wakala utafikia malengo kusudiwa ya mradi.
Hata hivyo Dkt, Sophia Kashenge aliyapongeza makampuni yanayozalisha Mbegu kwenye Mashamba ya Wakala kuendelea kutoa ushiriano ilikuweza kufikia Malengo ya Serikali.
Alisema kwamba Wakala wa Mbegu pamoja na makampuni ya Uzalishaji katika Mashamba ya Wakala Kwa pamoja wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha Uzalishaji unaongezeka.