Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Gervais Nyaisonga (kulia) wakati wa mazungumzo yaliyohusisha viongozi wa dini na serikali kuelekea katika mkakati wa kuunganisha nguvu ili kupambana na uhalifu,mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akisalimiana na Mkuu wa Kanisa Kuu la Kiinjili na Kilutheri(KKKT),Askofu Dkt.Alex Malasusa wakati wa mazungumzo yaliyohusisha viongozi wa dini na serikali kuelekea katika mkakati wa kuunganisha nguvu ili kupambana na uhalifu,mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Daniel Sillo akisalimiana na Mkuu wa Kanisa Kuu la Kiinjili na Kilutheri(KKKT),Askofu Dkt.Alex Malasusa(kulia) wakati wa mazungumzo yaliyohusisha viongozi wa dini na serikali kuelekea katika mkakati wa kuunganisha nguvu ili kupambana na uhalifu,mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini kutoka kulia ni Mchungaji Dkt.Barnabas Mtokambali, Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Gervais Nyaisonga na Mkuu wa Kanisa Kuu la Kiinjili na Kilutheri(KKKT),Askofu Dkt.Alex Malasusa na kutoka kushoto ni Naibu Mufti wa Zanzibar,Mahmoud Mussa na Mufti Mkuu wa Tanzania,Sheikh Abubakar Zubeir wakati wa mazungumzo yaliyohusisha viongozi wa dini na serikali kuelekea katika mkakati wa kuunganisha nguvu ili kupambana na uhalifu,mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Na Mwandishi Wetu,Dodoma
Katika kukabiliana na matukio ya uhalifu yanayotokea katika jamii tunayoishi Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefanya Kikao Maalumu na Viongozi wa Dini lengo ikiwa kuhusisha kundi hilo maalumu katika kudhibiti matukio ya uhalifu ikiwemo mauaji,mmomonyoko wa maadili,matumizi ya dawa za kulevya na matukio mengine yanayoweza kuvuruga amani ya nchi.
Akizungumza katika Kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya wizara Mtumba jijini Dodoma,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amewaomba viongozi hao wa dini kuendelea kuisaidia serikali katika kudumisha amani na usalama,akiwaomba kutochoka kutoa ushauri kwa serikali katika kudhibiti matukio ya uhalifu yanayoweza kuvuruga amani ya nchi huku akikiri kuwepo kwa upungufu wa uhalifu nchini akiwaomba viongozi hao kuiunga mkono serikali katika adhma yake ya kumaliza kabisa uhalifu.
‘Wajibu wa Jeshi la Polisi ni kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao unaimarika na amani inatawala nchini ili kuwezesha wananchi kufanya kazi zao za kiuchumi na kijamii na katika kutekeleza wajibu huo Jeshi la Polisi ushirikiana na jamii na wadau wengine na katika kipindi cha Julai,2023 hadi April,2024 makosa makubwa ya jinai yaliyoripotiwa katika Vituo vya Polisi yamepungua kutoka 45,485 hadi 43,146 sawa na asilimia tano ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka 2022/2023,kwahiyo nawaomba viongozi wa dini mkaiunge serikali mkono katika sehemu zenu mnakotoka kukemea na kudhibiti uhalifu’ Alisema Waziri Masauni
Akizungumza wakati wa kikao hicho,Mufti Mkuu wa Tanzania,Sheikh Abubakari Zubeir aliipongeza serikali kwa uamuzi wa kuhusisha viongozi wa dini katika mapambano dhidi ya uhalifu huku wakiitaka serikali kutochoka kuwaita yanapotokea matatizo mbalimbali ili kuendelea kuimarisha uhusiano huo.
‘Sina kumbukumbu kama tuliwahi kukaa hivi kujadili masuala ya uhalifu tangu wakati wa viongozi wetu wa zamani ila kwa hatua hii ya kuamua kutuita viongozi wa juu wa dini umefanya jambo la maana sana mheshimiwa Waziri na nikupongeze wewe na wenzako kwa wazo hili ambalo sasa linaenda kufungua milango ya mahusiano kati ya serikali na taasisi hizi za dini katika mapambano dhidi ya uhalifu.’ alisema Sheikh Zubeir
Akizungumzia usajili wa taasisi za kidini, Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Gervais Nyaisonga amesema serikali ipitie upya katiba za vikundi mbalimbali vya kidini kwani kupitia katiba zao ndio serikali itajua msingi wa shughuli za taasisi hizo za kidini ili kuepusha baadhi ya uhalifu ambao pia unatokea katika baadhi ya taasisi au vikundi vya kidini.
Naye Mkuu wa Kanisa Kuu la Kiinjili na Kilutheri(KKKT),Askofu Dkt. Alex Malasusa alisema wanaishukuru serikali kwani sasa wamepata mahali kama viongozi wa dini ambapo wanaweza kuzungumza na kuweka mikakati ya pamoja katika mapambano dhidi ya uhalifu na kukubaliana juu ya maazimio yaliyofikiwa ili kuona nchi inakua na amani na usalama.