MENEJA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma Bw.Mwita Ayubu,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Mei 17,2024 jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya TRA katika Mkoa wa Dodoma kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Na.Alex Sonna-DODOMA
KATIKA kipindi cha Miaka Mitatu ya Dodoma na Samia,Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma, makusanyo ya kodi yameongezeka kutoka wastani wa Shilingi Bilioni 15.19 hadi Shilingi Bilioni 18.71 kwa mwezi kuanzia mwaka 2021.
Hayo yameelezwa leo Mei 17,2024 jijini Dodoma na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma Bw.Mwita Ayubu,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya TRA katika Mkoa wa Dodoma kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inayofanyika katika Ofsi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Na kuongeza kuwa sababu za kuongezeka kwa makusanyo ya kodi ni pamoja na Uboreshaji wa mahusiano kati ya TRA na walipakodi,Mbinu bora za ukusanyaji na rafiki kwa mlipakodi,Uhamasishaji kwa kupitia elimu kwa mlipakodi na Ongezeko la matumizi ya mifumo ya Teknolojia na Habari na Mawasiliano yaani(TEHAMA).
“Mafanikio katika makusanyo ya kodi,kuanzia mwaka 2021 makusanyo ya kodi yameongezeka kutoka wastani wa Shilingi Bilioni 15.19 hadi Shilingi Bilioni 18.71 kwa mwezi.
“Makusanyo ya kodi kwa kipindi cha miaka mitatu mwaka 2020/2021 Shilingi 182,359,010,000.00, mwama 2021/2022 Shilingi 189,441,040,000.00 na mwaka 2022/2023 Shilingi 224,610,336,471.06”.
“Sababu za kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kwanza ni Uboreshaji wamahusiano kati ya TRA na walipakodi,ambapo ilikuwa ni maelekezo ya Mhe Rais,Mbinu bora za ukusanyaji na rafiki kwa mlipakodi,Ongezeko la uwekezaji na ukuaji wa shughuli za kiuchumi ikiwemo uzalishaji viwandani na sekta za ujenzi na usafirishaji,Ongezeko la matumizi ya mifumo ya Teknolojia na Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika usimamizi wa kodi, kuongezeka kwa hamasa ya ulipaji kodi kutoka kwa wananchi na Uhamasishaji kwa kupitia elimu”.
Aidha Meneja Ayubu amegusia Mafanikio katika matumizi ya mashine za EFD pamoja na kuelezea Faida za kutumia mashine hizo ambapo amesema kwa mujibu wa Sheria mtu yeyote anayefanya biashara binafsi/kampuni/ushirika ambapo anajihusiha na kuuza bidhaa au huduma anatakiwa kwa mujibu wa sheria kuhakikisha ananunua mashine ya EFD.
“Kwa mujibu wa sheria mtu yeyote anayefanya biashara binafsi/kampuni/ushirika n.k ambapo anajihusisha na kuuza bidhaa au huduma anatakiwa kwa mujibu wa mujibu wa sheria kuhakikisha ananunua mashine ya EFD/VFD, toka kwa Mawakala walioidhinishwa na TRA na kuitumia mashine hiyo kutoa risiti kila anapofanya biashara katika kuhakikisha anawatendea haki wateja wake kwa kuwapa rising sahihi”.
“Na kuongeza kuwa faida za kutumia .Ashington za EFD ni kuboresha ubora wa kumbukumbu za biashara kwa njia ya kielektroniki ambayo ni salama na yakiaminika,kuwepo kwa uwazi kati ya mlipakodi na Mamlaka mapato kupitia uhamishaji wa kielektroniki wa taarifa za mauzo,kutoa nafasi ya wafanya biashara kutendewa haki na Mamlaka na kupunguza migogoro ya kodi na kurahisisha upatikanaji wa kumbukumbu za biashara,”
Pia amezungumzia mafanikio katika shughuli zausimamizi wa kodi ambapo amesema Mkoa wa Dodoma umefanikiwa kupata nyongeza ya Watumishi wapatao 78 ambao wamekuwa chachu kubwa katika kuimarika kwa shughuli za makusanyo ambapo ongezeko hilo halijawahi kutokea.
“Katika kipindi cha miaka mitatu ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,Mkoa wa Dodoma tumefanikiwa kupata nyongeza ya Watumishi wapatao 78 ambao wamekuwa chachu kubwa katika kuimarika kwa shughuli za makusanyo. Ongezeko hili halijawahi kutokea kwa kipindi kama hiki katika historia ya Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Dodoma. Kipekee kabisa tunamshukuru Mh Raisi kwa ajira hizi mpya ambazo zimeimarisha utendaji kazi wa TRA katika Mkoa wetu wa Dodoma.