Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyoambatana na uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29) iliyofanyika Leo Mei 15,2024 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa,akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyoambatana na uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29) iliyofanyika Leo Mei 15,2024 jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana,akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyoambatana na uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29) iliyofanyika Leo Mei 15,2024 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyoambatana na uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29).
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Seif Shekalaghe, akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyoambatana na uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya, akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyoambatana na uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29).
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima,(hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyoambatana na uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29) iliyofanyika Leo Mei 15,2024 jijini Dodoma.
Wadau Mbalimbali wakitoa salamu kwenye Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyoambatana na uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29) iliyofanyika Leo Mei 15,2024 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima,akiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa,akizindua Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29) iliyofanyika Leo Mei 15,2024 jijini Dodoma.
PICHA ZOTE NA ALEX SONNA
Na WMJJWM, Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amesema mifarakano katika familia ina athari kubwa kwenye malezi na makuzi ya watoto.
Waziri Dkt. Gwajima ameyasema hayo Leo Mei 15, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyoambatana na uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29).
Amesema Jamii hususani Wazazi na Walezi wanatakiwa kuona umuhimu wa kumaliza tofauti zao, kudumisha upendo na amani katika familia kwa kuwa changamoto za migogoro ya ndoa inazidi kushamiri na kusababisha athari kubwa hasa kwa watoto.
“Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024 nimepokea taarifa mpya nchi nzima kwamba, takribani familia 30,000 zilitoa taarifa Ofisi za Ustawi wa Jamii kuwa na migogoro katika ndoa na mahusiano kutokana na sababu mbalimbali.” Amesema Dkt. Gwajima
Dkt. Gwajima amebainisha kwamba lengo la maadhimisho ya siku hiyo ni kutathmini nafasi ya familia katika ustawi, maendeleo na Taifa kwa ujumla na Idadi hii ni kubwa sana, lakini bado wako wengine watakuwa walikaa kimya bila kutoa taarifa; hili ni tatizo kubwa, tunahitaji nguvu ya pamoja ili kuimarisha familia zetu ambao ndio msingi wa Taifa Imara.
Amesema moja ya chanzo cha migogoro ya familia ni vitendo vya ukatili vinavyofanywa hususani kwa kundi la wanawake na watoto, akinukuu taarifa ya utafiti wa hali ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria nchini ya mwaka 2022 inayoonesha asilimia 27 ya wanawake wa umri wa miaka 15 hadi 49 walifanyiwa vitendo vya ukatili wa kimwili. Aidha, asilimia 12 ya wanawake wa umri huo walifanyiwa ukatili wa kingono.
Kuhusu uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) awamu ya pili, Waziri Dkt..Gwajima amesema Shabaha za Mpango wa kwanza ilikuwa kupunguza vitendo vya ukatili kwa zaidi ya nusu ambapo kabla ya kuanza kwa mpango huo mwaka 2015 ukatili wa kimwili kwa wanawake ulikuwa asilimia 40 na ukatili wa kingono ulikuwaasilimia 17.
Waziri wa Ofisi ya Rais-Tamisemi, akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema ofisi hiyo itaendelea kutekeleza afua za kupinga ukatili kupitia Sera zilizoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwenye tmTawala za mikoa na Serikali za mitaa.
“Utendaji utapimwa kulingana na namna ambavyo mhusika atapunguza matatizo katika jamii hivyo inabidi watendaji wapambane katika kupunguza ukatili na itaandikwa barua katika kila Mkoa, Halmashauri na kata nitakayoielekeza kusimamia ipasavyo mpango wa kutekeleza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA II)” amesema Mhe. Mchengerwa.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Seif Shekalaghe amesema Mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili kwa wanawake na Watoto awamu ya pili (MTAKUWWA II) ni mwendelezo wa juhudi za Serikali katika kupinga na kuondokana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambapo amekumbusha jukumu la malezi kwa watoto ni la wazazi hivyo jamii yapaswa kubadilika na kuupinga ukatili kwa nguvu zote.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesisitiza umuhimu wa kuepuka ukatili kwa wanafamilia ili kutunza amani na upendo katika familia na kuwaomba viongozi wa dini kuwafundisha vijana namna ya kuimarisha ndoa ili wasikimbilie kuvunja ndoa kirahisi.
Maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Familia yamebebwa na kaulimbiu isemayo “Tukubali tofauti zetu kwa malezi ya watoto” ambapo Wizara ya Maendeleo ya Jamii imeungana na mkoa wa Dodoma sambamba na uzunduzi wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto awamu ya pili.