Na Gideon Gregory, Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amesema kwa mwaka uliopita miongoni mwa iliyoongoza kuwa na ajali nyingi za barabarani ni Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Kagera ambapo jumla zilikuwa 163,148 jambo linalopekea kuyumba kwa uchumi wa famailia za wahanga na mzigo kwa taifa.
Dkt. Jingu ameyasema hayo leo Mei 11,2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza na maafisa usafirishaji kwenye kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Afya kuhusu namna ya kujikinga na ajali za barabarani ambapo ameongeza kuwa kuanzia mwezi Julai 2023 hadi Julai 2024 Serikali ilitumia zaidi ya milioni 20 kuwatibia majeruhi.
“Mtu akipata ulemavu wa kudumu hata kama sio wa kudumu lakini kipindi ambacho atakaa hospitalini bado atakuwa mzigo kwa familia pia na kwa Serikali”,amesema.
Amesema hata kwao ni mzigo mkubwa ambapo ametaja katika mwaka mmoja kuanzia mwezi Julai 2023 hadi mwezi kama huo 2024 katika Hospitali Nane tu za rufaa hapa nchini za Iringa, Shinyanga, Musoma, Mwanza, Manyara, Kitete na Simiyu mejeruhi wengi wa ajali walikuwa hawana hela za kugaramikia matibabu wala Bima za afya ilibidi wapewe msamaha wa matibabu.
Aidha Dkt. Jingu ameongeza kuwa kwasasa ajali za barabarani zimeongezeka kutokana na vijana wengi kutokuzingatia sheria za barabarani jambo linalopekea familia nyingi kupoteza nguvu kazi na kubakia kuwa tegemezi.
“Ndugu zangu wa bodaboda kwasasa inaonekana chati inaendelea kuongezeka na inaumiza kwani unakuta ni kijana ambaye anategemewa na familia yake na ana chombo ambacho ni halali anatumia kutafuta kipato ana mke na ana mtoto unakuta mwingine kaoa juzi juzi bado unabakia kuwa mzigo mkubwa”, ameongeza.
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Tumaini Nagu amesema maafisa usafirishaji kwa pamoja wanapaswa kuungana na kuseme kwasasa ajali Tanzania basi kwani wai ndio wadau muhimu katika sekta ya usafirishaji na hilo linawezekana.
Nao baadhi ya washiriki katika kikao hicho wameshauri kuwa ili ajali ziweze kupungua elimu inapaswa kutiliwa mkazo kwa maafisa usafirishaji kutokana na vijana wengi kuingia kwenye sekta hiyo.
“Elimkubwa ni muhimu kuendelea kutolewa ukiangalia kwasasa kila kukicha sura mpya zinaingia Barabarani ila hawana ujuzi wowote kwahiyo tunadhani kupitia msisitizo na mkazo wa kutoa elimu mara kwa mara itasaidia pakubwa kupunguza hizi ajali za mara kwa mara zinazokuwa zinajitokeza kila siku,”wamesema.