Na Fauzia Mussa, Maelezo
Mwenyekiti wa baraza la madiwani Wilaya ya kati Said Hassan Shaaban amesema baraza la mji kati limepanga mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya hiyo.
Ameyasema hayo katika kikao cha madiwani wa wilaya hiyo kilichofanyika Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na ujenzi wa vituo vya daladala ambapo tayari vituo kumi vimeshajengwa na vipo katika hatua ya mwisho ili kuanza kutumika.
Aidha ameeleza kuwa Baraza hilo limejipanga kuiendeleza miradi ya masoko iliyojengwa katika Wilaya hiyo pamoja na bustani zinazotarajiwa kutengenezwa katika maeneo ya Hanyegwamchana na Tunguu.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa baraza la mji kati, mkuu wa idara ya rasilimali watu, mipango, utawala na mtumzaji kumbu kumbu Rehema Khamis Hassan amesema watahakikisha kuwa wafanyakazi wa baraza hilo wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ili kufikia malengo yaliokusudiwa.
Aidha amesema watahakikisha ofisi ya baraza la mji kati inatekeleza miradi yote ya kimkakati ambayo imewekwa sambamba na uimarishaji wa miji katika robo ya mwaka inayomalizia 2024_2025.
kikao hicho ni cha tatu Kufanyika katika Baraza la tano la madiwani ndani ya Wilaya hiyo.
PICHA KWA HISANI YA BARAZA LA MJI KATI